Ukatili!!!!! MWANAMKE AKATWA TITI LAKE LA KUSHOTO ,WAUAJI WATOWEKA NA TITI HILO KUSIKOJULIKANA


Ukatili dhidi ya wanawake umeendelea kufanyika katika jamii ambapo huko mkoani Simiyu mwanamke mmoja aitwaye Minza Noni (56) ameuawa  kikatili kwa kukatwa mapanga titi lake la kushoto na watu wasiojulikana kisha kutokomea nalo kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia siku ya Jumamosi wiki iliyopita majira ya saa sita usiku katika kitongiji  cha Nyasiri kijiji cha Isiyu kata ya Girya wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Mkuu wa upelelezi  mkoa wa Simiyu ACP Evance Mwijage amesema mwanamke huyo  akiwa nyumbani kwake alivamiwa na kukatwa mapanga na watu hao kisha kumkata panga kwenye titi lake la kushoto na kutoweka nalo kusikojulikana na kwamba  jeshi hilo la polisi  linaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post