Katika kile kinachoweza kusimuliwa na wakazi wa mkoa wa Shinyanga kama
historia ama wengine kudhani pengine ni kama ndoto,hatimaye kiwanda cha nyama cha Triple ‘S’
kilichopo ndani ya manispaa ya Shinyanga ambacho kilichojengwa mwaka 1975 na hakijawahi kufanya
kazi hata siku moja kinatarajiwa kufunguliwa na kuanza kufanya kazi mwezi machi
mwaka huu.
Akizungumza jana mbele ya waziri wa
maendeleo ya mifugo na uvuvi Titus Kamani wakati wa ziara
yake mkoani Shinyanga alipotembelea
kiwanda hicho mmiliki wa kiwanda hicho Salum Seif amesema anatarajia kufungua na kuanza
kazi mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa kiwanda hicho kina uwezo kwa kuchinja ng’ombe
250 hadi 300 kwa siku ila kwa kuanza wataanza na ng’ombe 50 kila siku.
Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi Titus Kamani alitumia
fursa hiyo
kuwataka wafugaji watumie kiwanda cha nyumbani kinachoweza
kuchukua mifugo yao pamoja na kuwepo kwa changamoto ya ng’ombe wa hapa nchini kukosa ubora wa
kuingia kwenye ushindani wa soko la nyama hivyo kuwataka wafugaji kubadilisha
mfumo wa ufugaji na kuwa wa kibiashara ili waweze kunyanyua uchumi
wa mkoa wa Shinyanga na mtu mmoja mmoja.
Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Anna Rose Nyamubi alimtaka mwekezaji huyo kuwaelimisha wananchi walio
kando kando ya kiwanda hicho kwa kupitia afisa maendeleo ya jamii
kwa kutenga maeneo ya kuendeleza shughuli zao ili kuweza kuepusha
migogoro isiyokuwa ya lazima pia wafugaji nao kuelimishwa ili waweze kunufaika na kiwanda
hicho.