MWANAMKE RAIA WA UINGEREZA AJIFUNGULIA BARABARANI MJINI YORK,WAPITA NJIA WATOA MSAADA

Cian na mkewe tayari wana watoto wawili
Mwanamke mmoja raia wa Uingereza amejifungulia katika barabara moja mjini New York akiwa njiani kuelekea hospitali kutokana na uchungu wa uzazi.

Polly McCourt, mwenye umri wa miaka 39,aliondoka nyumbani kwake katika mtaa wa East Side siku ya Jumatatu na kujaribu kukodisha taxi hadi alipogundua kuwa mwanawe asingeweza kusubiri.
Wapita njia walimpa mama huyo koti na vitambaa walivyokuwa navyo kumfunika mwanawe hadi wahudumu walipofika kumsaidia na kumpeleka hospitaliini.
Mama na mtoto walikuwa salama walipofikishwa hospitalini.
"alipiga mayowe akisema Mungu wangu mtoto wangu yuaja ,'' alisema shahidi mmoja.
Na niliweza kuona kichwa cha mtoto. Tulipomlaza mama chini kumsaidia, mtoto akawa tayari ametoka.''
Bi McCourt, anayetoka nchini Uingereza alijifungua mwanawe kando ya barabara.
Mama huyo alionekana akitabasamu alipoingia katika gari la ambulensi na kupelekwa katika hospitali ya Lennox Hill mjini New York.
Mumewe mama huyo alikuwa amekwama barabarani kutokana na msongamano wa magari alipopata simu kutoka kwa mkewe.
Wawili hao tayari wana watoto wengine wawili, Conor mwenye umri wa miaka sita na Adele mwenye umri wa miaka minne kulingana na jarida la New York Daily News.
Inaarifiwa walihamia mjini New York miaka minne iliyopita kutoka Dublin nchini Ireland.
>>via bbc swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post