Breaking News!!! BASI LA BUNDA EXPRESS LAGONGA TRENI HUKO SINGIDA

Eneo la tukio


Habari kutoka Manyoni  mkoani Singida zinasema kuwa Basi la Bunda Express lililokuwa linatoka Dodoma kuelekea Mwanza limegonga  Treni iliyokuwa inatoka Aghondi Itigi katika eneo la njia panda ya Itigi Na Singida.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka eneo la tukiokinasema kuwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Bi Kombo amefariki dunia na kadhaa kujeruhiwa.

Majeruhi 38 tayari wamepelekwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

 
Chanzo cha ajali inasemekana kuwa ni uzembe wa dereva ambapo inadaiwa dereva wa gari hakusimama wakati anajua anapaswa kusimama katika eneo hilo la njia ya treni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post