MTOTO WA MIAKA MINNE ATUMBUKIA CHOONI NA KUFARIKI DUNIA HUKO TABORA

Mwili wa mtoto John Mwapwani (4)aliyefariki majira ya  asubuhi baada ya kutumbukia kwenye tundu la choo nyumbani kwao mtaa wa Sikanda kata ya Chemchem eneo la Ally Hassan Mwinyi ndani ya Manispaa ya Tabora.

Inasemekana kuwa mtoto huyo mara baada ya kuamka asubuhi ,baba yake mzazi alimwambia aende chooni kujisaidia kama ilivyo ada kwa wazazi wafanyavyo kwa watoto wao,Mtoto John(4)alikwenda chooni.

Baada ya kimya  cha muda mrefu kutawala baba wa mtoto huyo alielekea sehemu ya choo,lakini katika hali ya kusikitisha alikuta mwili wa mtoto huyo ukielea kwenye maji machafu akiwa tayari amepoteza maisha.

Picha na kapipij blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post