Katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi
wa shule ya Sekondari Nyugwa iliyoko katika kijiji cha Mimbili kata ya Nyugwa
wilaya ya Nyangw'hare mkoani Geita wameiomba serikali ya mkoa kuwachukulia hatua
afisa elimu wa sekondari wa wilaya Bi Mosha pamoja na mkuu shule hiyo Lucas
Joshua kwa kuuza majina yao na kuwalazimisha kuwapa majina yasiyokuwa yao
wakati wana majina yao tena kwa kuyanunua kwa pesa.
Wakiongea kwa nyakati tofauti jana ,wanafunzi
hao wamesema mkuu wa shule hiyo Lucas
Joshua amekuwa ni kinara wa kuuza majina yao na kuwapa majina yasiyokuwa
ya kwao na kuwataka kama wanataka ya kwao yaliyopotea kutakiwa kuyanunua kuanzia
kiasi cha shilingi elfu 25 hadi elfu 30 kwa
madai kuwa majina yao ya awali yanafuatwa mkoani kwa pesa.
Wanafunzi hao wamesema mwalimu huyo pamoja
na kuuza majina yao amekuwa na tabia mbaya sana katika shule hiyo kwa kufuja
mali za shule bila kufuata utaratibu.
“Kwa kweli hatupendi tabia za mwalimu
mkuu,mbaya zaidi amekuwa akisema hakuna mtu yeyote wa kumgusa hata awe nani na
yeye ndiyo mkuu na mwanafunzi ambaye hataki kutumia jina lililopo aache “,
walisema wanafunzi hao.
Kwa upande wake mkuu huyo wa shule alipoulizwa
kuhusu tuhuma hizo alisema yeye si
msemaji na msemaji ni afisa elimu wa wilaya lakini pamoja matukia hayo cha
kushangaza wanafunzi 11 waliofanya mtihani wa kuingia kidato cha tatu mwaka
jana walifanya mtihani wao kwa kulazimishwa kutumia picha na majina
yasiyo ya kwao na Afisa elimu wa wilaya hiyo Bi Mosho.
Akizungumzia kuhusu tuhumu hizo afisa
elimu wa sekondari wa wilaya Bi Mosha alikiri kulifahamu suala hilo na kuhusu
kuwafanyisha mtihani wanafunzi kwa majina yasiyokuwa ya kwao alidai kuwa aliamua kufanya hivyo hili asivuruge mtihani
uliokuwa ukiendelea na kuahidi kulishugulikia suala hilo kwa kumchukulia hatua
kali mwalim huyo.
Naye Diwani wa kata ya Nyugwa katika
wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita Charles Kabosoro akiongea na wanafunzi wa
Shule ya sekondari Nyugwa wakiwemo wanafunzi waliopewa majina ya bandia ya
kufanyia mtihani wa kidato cha pili mwaka jana ambao walimwita pamoja na wazazi
ili kujua hatma ya kutopewa majina yasiyokuwa yao,amelaani kitendo hicho cha mwalim huyo pamoja na afisa elimu wa
wilaya kuhujumu majina ya watoto wao na kuwalazimsha kuwapa ya majina ya bandia
na kuiomba serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika bila kujali mtu
yeyote.
''Mimi kama diwani kata hii naona hata afisa
eliu anahusika kwani angekuwa hahusiki
asingewambiwa wanafunzi wafanye mtihani kwa majina bandia kwa kulazimishwa na
yeye na kuahidi kulichukulia hatua na mpaka sasa hajachukua hatua naye anahusika”,alisema
diwani huyo.
Kitendo hicho cha kuuzwa kwa majina ya watoto
kuuzwa na kupewa majina ya bandia kimewashangaza wakazi wa mkoa wa Geita pamoja
na vitongoji vyake huku wanafunzi waliopewa majina bandia wakiwa hawajui pa kwenda.
Na Valence Robert-Geita