Updates!! MWANAMME ALIYECHINJA MKE WAKE KISA KUNYIMWA UNYUMBA HUKO TABORA AFARIKI DUNIA


Mwanamme aliyedaiwa kumuua kwa kumchinja mke wake huko katika kijiji cha Tazengwa mkoani Tabora majira ya saa 7 usiku wa Februari 16 mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba mara kwa mara naye amefariki dunia kufuatia majeraha aliyokuwa nayo shingoni .

Habari kutoka Nzega zinasema kuwa mwanamme huyo mkazi wa kijiji cha Tazengwa wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Juma Kiyabo (45) alimchinja mke wake, Wande Monera (34),amefariki dunia juzi jioni wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Nzega.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post