Updates!! KIJANA ALIYEUA MAMA YAKE KWA JEMBE ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA

Yule kijana aliyemuua mama yake kwa kumkata jembe kichwani juzi na kusababisha kifo chake papo hapo huko katika kijiji cha Mwakuhenga wilayani Kahama mkoani Shinyanga anashikiliwa na jeshi la polisi.

Kaimu kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, mrakibu mwandamizi wa Polisi, Juma amemtaja mwanamke aliyeuawa kuwa ni Munde Luchagula (48-50) ambaye alikatwa jembe na mwanaye Mbogo Charles (34) wakati akiandaa chakula cha usiku.


Amesema chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika japokuwa inahisiwa mtuhumiwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili na tayari anashikiliwa na jeshi la polisi na atapimwa ili kubaini ukweli 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post