Inasikitisha!!! MWANAMKE AFARIKI DUNIA AKIWA GESTI NA MPENZI WAKE HUKO GEITA

Katika hali ya kusikitisha mwanamke mmoja  aliyejulikana kwa jina la Christina Charles (20) mkazi wa Kharumwa  mkoani Geita amefariki dunia akiwa Guest(Nyumba ya kulala wageni) akiwa na mpenzi wake Mniry Masii mfanyakazi wa kituo cha afya cha Kharumwa katika halmashauri ya wilaya Nyang’hwale mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika Nyumba ya kulala wageni  iliyopo mjini Nyang’wale inayojulikana kwa jina la Saju Guest house.

Imedaiwa kuwa siku hiyo mtuhumiwa ambaye ni mfanyakazi wa kituo hicho  cha afya ambaye ni katibu wa kituo cha afya Kharumwa anayefahamika  kwa jina la Mniry Masii alimchukua Christina Charles(20) ambaye ni mkulima muda wa saa tatu usiku na kwenda naye katika gesti hiyo na kupewa chumba kwa ajili ya kupumzika.

Habari zinasema kuwa  ilipofika saa 7 usiku mhudumu wa gesti hiyo aliitwa na (Mniry Masii) mtuhumiwa huyo aende kwenye chumba chake na alipofika alimkuta huyo mama anatoa mapofu na mtuhumiwa akiwa amekaa pembeni huku akilia....

Mhudumu  alipomuuliza mwanamme(Mniry Masii) kulikoni!! ,hakujibu chochote zaidi ya kuendelea kulia kutokana na kutojibiwa  yule mhudumu alirudi alikokuwa.

Imeelezwa kuwa mhudumu huyo wa gesti  aliporudi na kulala baada ya muda mfupi tena akaitwa  tena na bwana Mniry Masii akasema kuwa  mpenzi wake Christina amebanwa na kifua ,ndipo wakambeba na kumpeleka hospitali ya Kharumwa na walipofika tayari alikuwa amefariki dunia.

Diwani wa kata ya Kharumwa Marco Masusu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari mazishi yameshafanyika.

Hata hivyo inadaiwa kuwa mwanamke huyo enzi za uhai wake alikuwa na matatizo ya kuugua kifua na baadhi ya watu wamesema kuwa huenda hali ya hewa kulingana na tatizo hilo imepelekea kuweza kupoteza maisha katika hali aliyokutwa nayo.

Naye mama mzazi wa marehemu Bi, Salome Nkuji (30) ambaye ni mkazi wa Mwanza alipofika msibani alieleza kuwa  binti yake alikuwa na matatizo ya muda mrefu tangu azaliwe.

“ Binti yangu tangu nimzae miaka 20 iliyopita alikuwa na tatizo la kifua (athma)’’ ,alisema mama huyo bila ya kuongeza lolote.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani Geita Simon Pasua amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Mniry Masii (mtuhumiwa ) hajatenda kosa la kuua bali ni hali ambayo imetokea kama ambavyo mtu anaweza kuwa amelala na mtu mgonjwa halafu mauti yakampata .

“Ndugu mwandishi ni kweli tukio lipo lakini haya sio mauaji  ni mtu ambaye alikuwa anaumwa siku zake zimefika kwa hali hiyo na tulimshikilia mtuhumiwa tumemhoji na tayari tumeshamwachia”,alisema kamanda Pasua.

 Na Valence Robert-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post