Hot News!! SAKATA LA MADIWANI WA CHADEMA KUJIUZULU SHINYANGA,HII HAPA NDIYO TAARIFA KAMILI


Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinaynga kimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wawili katika manispaa ya Shinyanga kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na madai kuwa  viongozi ngazi ya taifa  wa chama hicho kundekeza  majungu,migogoro ,kudhalilisha baadhi ya viongozi  pamoja na  kuwapa majina ya wasaliti wa chama.

Madiwani  waliofikia maamuzi hayo magumu ni diwani wa Kata ya Ngokolo Sebastian Peter maarufu OBAMA WA NGOKOLO na Zacharia Mfuko wa kata ya Masekelo  ambao wamesema wameamua kufikia maamuzi hayo magumu kama ishara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho kitaifa.

Madiwani hao wawili tayari wameshakabidhi barua za kung’atuka nafasi zao katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga

Hili   ndiyo barua ya tamko la diwani wa Ngokolo Sebastian Peter kuhusu kujiuzulu nafasi yake ya udiwani aliyoikabidhi ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga ikielez sababu za kuchukua maamuzi hayo huku akisisitiza kuwa atabaki kuwa mwanachama mwadilifu wa Chadema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post