Ni Balaa!!! SHUHUDIA HAPA ZIARA YA RC SHINYANGA KWENYE VIWANDA VYA WACHINA ,TAZAMA PICHA KIBAO ZA VIWANDA HIVYO

ZIARA ILIANZA HIVI-Ziara ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(aliyevaa suti hapo mbele) jana akiwa ameambatana na wataalam mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga na mkoa pamoja na waandishi wa habari kutembelea na kujionea hali ya maendeleo ya ujenzi viwanda vitatu vinavyojengwa mjini Shinyanga yaani kiwanda cha ngozi na nyama,kiwanda cha nyuzi za pamba na kiwanda cha mafuta yanayotokana na mbegu za pamba na alzeti.Ziara ilianzia  katika kiwanda cha nyama na ngozi kiitwacho  Xing Hua company Limited kilichopo eneo Ibadakuli mjini Shinyanga.Hapo anapokelea na viongozi wa kiwanda hicho baada ya kuwasili katika eneo la kiwanda hicho

NDANI YA KIWANDA CHA KWANZA-Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga (mwenye suti katikati ) akipata maelezo kutoka kwa mkalimani wa kiwanda hicho  bwana Wu Yu kuhusu kiwanda hicho ambacho cha ngozi(mbuzi,kondoo na ng'ombe) na nyama ambacho pindi kikianza watu takribani 500 watapata ajira kipaumbele wakiwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga na kwamba hivi sasa wana vibarua wenyeji 30 katika hatua ya awali.Kiwanda hicho  kinatarajiwa kuanza kufanya kazi kabla ya mwezi Julai mwaka huu.Tayari wameshaanza kukusanya ngozi kama unavyoona kwenye picha.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga pamoja na msafara wake wakiangalia dramu takribani 14 ambazo zinatumika katika shuguli nzima ya kuchanganya nyama ambapo kwa mujibu wa wachina hao walisema wataweza kuzalisha vipande vya nyama kuanzia elfu 10 hadi 15 kwa siku na baada ya kuzalisha nyama hizo zitahifadhiwa pamoja kuuzwa ,huku ngozi zikitumikwa ajili kutengenezea bidhaa mbalimbali kama vile viatu,mikanda n.k

KIWANDA CHA PILI-Mkuu wa mkoa wa Shinyanga anapokelewa na mkalimani wa kiwanda cha nyuzi za pamba bwana Simon Zhou(katikati) pamoja na mtoto wa mwekezaji ( wa pili kutoka kulia) wa kiwanda cha  Dahong Textile(Tanzania) Co.Ltd kilichopo katika eneo la Nhelegani mjini Shinyanga.Kiwanda hiki kinatarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi March  mwaka huu ambapo kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,kiwanda hicho kitafunguliwa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.Kiwanda hicho kinaendeshwa kwa kutumia mashine za kisasa na watu 80 watapatiwa ajira

Hizi ni spinning machine kwa ajili ya kutengezea nyuzi za pamba.Ambapo kwa mujibu wa mkalimani wa bwana Simon Zhou Pamba inayozalishwa kanda ya ziwa itapewa kipaumbele zaidi katika kuhakikisha kuwa wanamsaidia mkulima kuinuka kiuchumi.Lakini pia alisema kiwanda hicho kitatoa mbegu,dawa na mbolea kwa wakulima kupitia mikataba watayowekeana

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiangalia mashine hizo,ambapo alisema serikali itashirikiana na wawekezaji hao katika kufikia malengo yanayotakiwa ikiwemo kuwapatia ajira wananchi lakini pia akawaomba wananchi wanaozunguka maeneo ya viwanda kuacha kuwaibia vifaa mbalimbali  wawekezaji hao kutokana na kuzuka kwa tabia za udokozi vinavyofanywa na watu wasio waaminifu.

KIWANDA CHA TATU- ni katika kiwanda cha Kutengeneza mafuta ya nayotokana na mbegu za pamba na alzeti(Jielong Holdings Tanzania Limited).Kulia hapo mbele ni mkurugenzi wa kiwanda hicho bwana Jerry Qi akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga (wa kwanza kutoka kushoto),ambapo alisema hivi sasa wanafanya majaribio kwa mashine zao na tayari wameshaajiri watu 80 na hadi kufikia mwisho wa mwaka huu wanategemea kuajiri watu wengine 100

Ndani ya kiwanda-Mkurugenzi mtendaji wa Jielong Holdings Tanzania Limited Jerry Qi akiwaonesha mabaki ya pamba katika kiwanda hicho na kuwaeleza kuwa hivi sasa wapo katika hatua za majaribio na mafuta yao yanayotokana mbegu za pamba yanaitwa URAFIKI PURE OIL(Urafiki Imara,Afya Imara).

Mashine mbalimbali zinazotumika katika uzalishaji wa mafuta katika kiwanda hicho

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post