 |
Bwana Chifu Abdalah Sube,Mwenyekiti wa mtaa wa Mbuyuni katika kata ya Ndembezi zilipo shule mbili za msingi ya Bugoyi A na B mjini Shinyanga akiangalia mfuko wa mahindi(huo wa mwanzo) ulioletwa katika shule ya Bugoyi A kwa ajili ya shule hizo mbili kugawana mahindi yaliyodaiwa kupelea katika magunia sita yaliyotolewa na diwani wa kata hiyo David Nkulila mwanzoni mwa wiki hii,ambapo magunia hayo(matatu kila shule) yalionekana kuwa na ujazo pungufu na kumlazimu diwani hiyo kumwagiza afisa mtendaji wa kata ya Ndembezi kwa kushirikiana na afisa kilimo wa manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa wanakabidhi mahindi yaliyopelea kwa mwenyekiti huyo wa mtaa haraka iwezekanavyo baada ya kuwepo harufu ya uchakachuaji wa mahindi hayo ambayo alinunua kwa ajili ya uji kwa wanafunzi wa shule tatu za msingi katika kata yake.Mwalimu mkuu wa shule ya Bugoyi A Selemani
Shaban Kipanya amesema amepokea mahindi hayo jana jioni majira ya saa 12 kwa ajili ya shule yake na Bugoyi B. |
 |
Mfuko huo wa mwanzo unaouona ndiyo ulioletwa kwa ajili ya kukamilisha ujazo wa magunia hayo sita,Akizungumza na Malunde1.blogspot.com mapema wiki hii diwani wa kata ya Ndembezi
David Nkulila ambaye pia ni naibu mstahiki
meya wa manispaa ya Shinyanga alisema kata ya Ndembezi hivi karibuni ilipata
magunia 197 ya mahindi ya msaada kutoka ofisi ya waziri mkuu kitengo cha
maafa yagawiwe kwa vijiji 19 vya kata
hiyo kwa ajili ya kupunguza makali ya njaa.
Alifafanua kuwa katika magunia hayo
197,yeye binafsi kama diwani wa kata hiyo aliamua kununua magunia 11 kwa ajili
ya kusaidia wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Bugoyi A na B pamoja na
shule ya msingi Ndembezi ili mahindi yatumike kwa ajili ya uji wawapo shuleni
huku magunia mengine yakigawiwa kwa wakazi wa kata hiyo.
“Lengo lilikuwa ni kutaka wanafunzi wetu
wapate uji bila ubaguzi, lakini pia kuwahamasisha wazazi kuchangia suala la uji
kwa watoto wao, nikawashirikisha wenyeviti wa vijiji wakakubaliana na wazo
langu, ,nikanunua magunia 11 kwa pesa zangu,kila gunia likigharimu shilingi
elfu tano lakini nashangaa kuona magunia haya yakiwa hayana ujazo
unaotakiwa,yako pungufu”,alieleza Diwani huyo.
|
 |
Malunde1.blogspot.com leo asubuhi ilifanikiwa kuona wanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A wakipata huduma ya uji katika eneo la shule hiyo |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment