NDEGE YA ZAN AIR YAANGUKA PEMBA WAKATI IKITUA,ABIRIA 17 WANUSURIKA KIFO


 Abiria 17 akiwemo waziri wa katiba na sheria Zanzibar Mhe. Abubakar Khamis Bakar, na marubani wawili, wamesalimika kifo jioni ya leo baada ya ndege ya shirika la ndege la ‘Zanz air’ kufeli breki, muda mfupi wakati ndege hio ilipo kuwa ikitua  kwenye uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume, uliopo nje kidogo ya mji wa Chakechake mkoa wa kusini Pemba.

Kwa mujibu wa tarifa zilizo tolewa na makamanda wa polisi mkoa kusini Pemba  kamishina msaidizi  swalehe mohamed swalehe na kamanda wa kikosi cha zima moto na uokozi pemba wamesema ndege hiyo wakati wa kutua ilipata ikhitilafu ya kufeli breki na kusereka hadi nje ya uwanja  umbali wa mita miambili kwenye vichaka

 Wamesema abiria wote wametoka salama hakuna alie juruhiwa    licha ya ndege hio kuacha uwanja kusereka kwenye nyasi na kungia kwenye mashamba ya muhogo kupita kwenye masiki majiti yalio katwa nakisha kusimama baada ya ringi kujizonga namizizi ya pori hilo.

 Ipo haja kwa mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kutoa taluma kwa watendaji wa kiwanja cha ndege kisiwani pemba kutoa ushirikiano kwa wandishi wa habari pale inapo tokea dharura kutokana na watendaji wa kiwanja chandege kisiwani hapa kushindwa kabisa kutoa usjhirikiano kwa wandishi juu ya tukio hili.
Credit-ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post