Ukatili !! NYWELE NDEFU ZAMPONZA MWANAFUNZI HUYU,AVUNJWA KIDOLE KWA UBAO NA MWALIMU WAKE-MBEYA

Mwanafunzi akiyevujwa kidole kwa ubao na mwalimu wake

Mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Aiport Kata ya Iyela jijini Mbeya Jacline Staniely[9]amefanyiwa ukatili na mwalimu wake kwa kupigwa ubao na kusababisha kidole cha mkono wake  wa kushoto kuvunjika kutokana kile kilichodaiwa mwanafunzi huyo kwenda na nywele ndefu shuleni .

Jacline akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.


Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika kumwambia mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa.
Hata hivyo Jackline amesema kuwa kutokana na maumivu makali alilazimika kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne bila kupata matibabu ya kutosha.

Baada ya kurejea kutoka safari mama yake mzazi aitwae Rehema Adamson Ndeje[28] mkazi wa Block T jijini Mbeya amesema baada ya maumivu ya mwanae usiku ilimlazimu kwenda shuleni ili kujua kulikoni,ndipo alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya kukutanishwa na Mwalimu mkuu.

Mama Jackine amesema hicho ni kipigo cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa na mwalimu huyo ambapo alionesha makovu yaliyodaiwa yalitokana na vipigo vya mwalimu huyo miguuni akidai majeraha hayo yalidumu kwa miezi mitatu.

Hata hivyo Rehema aliamua kwenda Polisi Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio na kila alipoitwa mwalimu huyo hakutokea ndipo jalada likapelekwa kituo kikuu cha kati ambapo mwalimu alikamatwa na mhanga kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu ambapo alipigwa picha na kuonekana moja ya kidole cha kati cha kushoto kuoneka kuathirika kutokana na kupigwa kwa kutumia ubao.

Mzazi huyo amesema hana niA mbaya na mwalimu Kanyika lakini kitendo cha kumwadhibu mwanae mara kwa mara ndicho kimemtia shaka hata kuamua kutoa taarifa Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
Mwandishi wa habari hii alipofika shuleni ili kujua mustakabali wa suala hili mwalimu alitoa nje mwandishi akidai yeye ana majukumu mengine lakini baada ya kufuatilia mkuu huyo alichukua gari lake aina ya RAV 4 na kwenda nyumbani kwa Mzazi wa mtoto na kwenda naye hospitali akiwa ameambatana na mmoja wa walimu wa shule hiyo ambaye ni jirani ambapo Jackline humwita Bibi.

Mwandishi alimtafuta mmoja wa wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri kupokea lalamiko hilo ingawa alijibu kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia kidogo tu na ni usanii mtoto huyo kufungwa POP na kwamba bado PF3 haijajazwa kitu hivyo hawezi kuzungumzia lolote.

Kumekuwa na malamiko mengi katika Dawati hilo kutokana na matukio kutochunguzwa kwa wakati hali inayotoa mwanya kwa vitendo hivyo kuibuka mara kwa mara na wahalifu kutoroka mkono wa sheria lakini baadhi kuwa na utendaji duni licha ya taarifa kutolewa kwa wakati.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ameahidi kulifuatilia suala hilo na ikibainika mtuhumiwea atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Na Ezekiel Kamanga -Mbeya

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post