Inasikitisha!!! MWANADADA AKATWA MIKONO NA MIGUU AKIFANYA JARIBIO LA KUONGEZA MAKALIO

http://www.theclicktz.com
http://www.theclicktz.com

Imetokea huko Amerika Dada mmoja anayeitwa Apryl Michelle Brown, ambaye alienda kuchoma sindano ya kuongeza makalio kwenye kituo fulani cha urembo na afya huko marekani alifanya hivyo kwakuwa hakuwa ameridhika na ukubwa wa makalio yake na kufanya uamuzi wa kutafuta mbinu ya kuyaongeza.

Dada huyo baada tu ya kuchoma sindano hiyo alikaa mwezi mmoja nakuanza kupata maumivu makali kwenye miguu yote miwili na mikono.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi na ilibainika kuwa sindano aliyochoma haikuwa sahihi na matokeo yake ilisababisha sumu mwilini, ambapo wataalamu walisema kuwa sindano hizo huchomwa kulingana na Mwili wa mtu pia aina na uwezo wa chembe chembe zake za damu.

 Inasemakana aliyechoma hakuangalia ni aina gani ya sindano ambayo ingeweza kuendana na mwili wa dada  huyo. 
Hivyo kumpelekea dada huyo kutopata nafuu na badae wataalamu kuamua kumkata Mikono yake na miguu. 

Dada huyo alivieleza vyombo vya habari kuwa " nitajutia maisha yangu yote kwa jambo nililo fanya". 

INASIKITISHA: WAKIDADA HILI NI FUNZO KWENU..!!

chanzo-clicktz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post