MKUTANO MKUBWA KUKABILIANA NA WAHAMIAJI HARAMU NA MAJAMBAZI WAANZA MKOANI GEITA

Na Valence Robert-Geita
Mkutano  mkubwa wa siku mbili wa kukabiliana na wahamiaji haramu pamoja na majambazi wanaotumia Silaha kutoka nchi zinazopakana na Tanzania umeanza kufanyika katika Mkoa wa Geita.


Akifungua mkutano huo leo katika ukumbi wa Alufa Hotel mjini Geita ,mgeni rasmi Mkuu wa mkoa  wa Geita Magalula Said amesema kuwa pamoja na kufanya mkutano uwo mafisa uwamijia wa Mikoa wanatakiwa kuwa makini kwani kuna maafisa ambao si waadilifu katika kazi zao ambao  wamekuwa wakipewa pesa na kurudisha nchini wahamiaji waliorudishwa kwao.

Naye kamishina utawala wa fedha kutoka makao mkuu Piniel Mgonja kwa niaba ya kamishina mkuu wa uhamiaji Tanzania amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa kukubali kuwa mgeni rasmi na kuongeza kuwa watahakikisha wanazingatia yote aliyoyasema Bw Magalula na kunogeza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua maafisa uhamiaji  wanaojihusisha na rushwa,

Mkuutano huo wa siku mbili unashirikisha  maafisa uhamiaji wa mikoa sita ambayo ni Shinyanga,Rukwa,Kigoma,Kagera,Katavi na Simiyu lengo kubwa likiwa ni kujadili jinsi ya kuendelea kupambana wahamijia haramu wanaorudi nchini baada ya oparesheni kimbunga kuisha


Mkutano huu ni wa pili kufanyika ndani ya mwaka huu na wa kwanza ulifanyika katika Mkoa wa Rukwa na wa pili umefanyika mkoani Geita na unatajia kuisha hapo kesho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post