SOMA HAPA SABABU KIBAO ZINAZOWEZA KUSABABISHA MAPENZI KUISHA /KUPUNGUA KWA UMPENDAYE


Kuna Sababu nyingi nana zinazoweza kusababisha mapenzi kupungua kwenye mahusiano yenu na wakati mwingine hata kusababisha kuachana. Zifuatazo ni sababu 10 kati ya sababu hizo;-

1.       UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.


2.       USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.


Kama kuna kitu hukuwahi kumwambia na unahisi ukimwambia atakasirika ni bora umtafutie nafasi nzuri umwambie kuliko aje kugundua mwenyewe itakuwa shida sana kukuelewa, kwa mfano mpo kwenye mahusiano mwaka wa 4 sasa na kumbe kabla ya kuwa na yeye ulishawahi kuoa/kuolewa na una watoto 2 kwa huyo mke/mume wa mwanzo ni bora umwambie kuliko kumficha, anaweza kukuelewa lakini mara nyingi ni kwa shingo upande.

3.       ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye love kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.
Huwa inauma sana na mara nyingi huwa inasababisha hata wengine kuweza kuondoka kwenye mahusiano hata kama walikuwa bado wanapenda pale walipo. Hakuna binadamu anayependa kuwa ‘’option’’ kwenye mapenzi. 


Kamwe Usimuumize Moyo Akupendaye Kiukweli, Usimfanye Ajutie Penzi Lako, Usimfanye Anung'unike Kwa Unayomtendea, Unaweza Kuona Ni Ujanja Lakini Ipo Siku Utahitaji Mapenzi Ya Kweli Kwa Mwingine Na Hutayapata, Laana Ya Mapenzi Ipo,  Ukimuumiza Ipo Siku Nawe Utaumia Tu, Mapenzi Ya Kweli Yanawezekana Kama Ukiamua na si kwa ku-cheat.

4.       DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa khali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.


Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri  au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo, ila wasichana wanatakiwa kutambua kuwa Linapokuja Suala La Ndoa/Kuishi Na Mtu, Kwetu Sie Wanaume Huwa Hatuangalii Uzuri/Urembo Wa Mwanamke Kama Ndio Kigezo Pekee Cha Kufanya Tumuoe/Tuishi Na Huyo Mwanamke, Ingekuwa Hivyo Basi Wanawake Wote Warembo/Wazuri Wangekuwa Ndani Ya Ndoa Leo Hii, Hii Inamaanisha Kuwa Hata Ukiwa Mrembo/Mzuri Hutakiwi Kujisahau Ukaona Umeshafika...Utapotea ukileta dharau kwa uzuri wako au uwezo ulionao.

5.       MROPOKAJI/ASIYE MSIRI.
Hakuna kitu kinachoweza kumfanya mwenza wako kukukimbia au hata kukosa uaminifu na wewe kama akija kugundua kama wewe ni mropokaji na huna ‘’kifua’’ hasa kwa yale mambo ambayo ni ya chumbani na hayakutakiwa kutoka nje. Hakuna mtu anayependa siri zake kutoka hadharani na huwa inaumiza sana kwenye mapenzi kumpa mtu siri zako then yeye anaenda kusimulia.


Mambo mnayafanya mkiwa wawili tena ndani lakini kesho unaenda mtaani unakuta kila mtu anajua mlichofanya tena wanakuhadithia kama walikuwepo vile, hiyo si kitu nzuri na itakufanya ukimbiwe na kila mpenzi unayempata.


6.       TAMAA/KUKOSA UVUMILIVU.
Tamaa ni kitu kingine ambacho hufanya mahusiano mengi kukosa nguvu na mengine kuvurugika kabisa. Kama mpo kwenye mapenzi na mmeamua kupendana kwa shida na raha basi haitakiwi mmoja wenu kuwa na tama na kukosa uvumilivu hata kwa yale mambo yanayoweza kuzuilika.


Kama mpenzi wako ni wa hali Fulani na umeamua kuwa naye basi usiwe na tama kwa vitu vingine ambavyo vinaweza kukusababishia mahusiano yako kukosa nguvu na kufa kabisa. Amini kuwa ipo siku mtakuwa na vitu kama unavyotamani kwa kuongeza bidii kutafuta na kushauriana nini cha kufanya lakini si kwa kutafuta ‘’shotcut’’/njia nyepesi nyepesi zinazoweza kuku-cost hapo baadae.

7.       KUKOSA MSIMAMO.
Hii kitu huwakuta wengi sana kwenye mapenzi ya siku hizi. Nadhani ni hali halisi ya dunia ya sasa inachangia pia pamoja na teknolojia tuliyonayo ya kutuwezesha kufanya yale tunayoyaona kwenye mitandao na vyombo mbali mbali vya habari.


Wapenzi wengi siku hizi wamekosa msimamo kwenye mapenzi/mahusiano yao na unakuta tu mmoja anakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na wanakuwa hawafahamiani huku kila mmoja akijua kuwa yeye ndo kila kitu kwa mpenzi wake.

8.       KUTOJALI/KUTOKUWA NA MSAADA.
Hii pia kwa kiasi kikubwa inaumiza sana na kupelekea kushuka kwa thamani ya mapenzi miongoni mwa mahusiano mengi haa duniani. Kama kweli unampenda mpenzi wako basi msaidie anapopata matatizo na umjali na kumchukulia kama mpenzi wako na mtu wako wa karibu na sio kukimbia majukumu bila sababu zote za msingi.


Kama huwezi kujali na kusaidia basi usiingie kwenye mahusiano ni bora ukae mwenyewe kuliko kuwepo sehemu usiyotakiwa.

9.       UBAHILI.
Huna sababu yoyote ya kuwa na pesa na mpenzi wako akawa anapata tabu kama vile humuoni. Sijasema utoe pesa hata kwa mambo yasiyo na msingi lakini at least utimize majukumu yako kwa mpenzi wako kila unapohitajika.


Kuna vitu vingine hata huhitaji kuambiwa kama unatakiwa kuvishughulikia, ni wewe mwenyewe tu kuwa responsible kumhudumia mpenzi wako. Na hii huwa ina-apply sana kwa wavulana kutokana na kasumba iliyojengeka na mila tulizozikuta.

10.   USHOGA/USAGAJI
Hii ipo wazi kabisaaaaaaa…. Hakuna mtu anayependa mtu wake awe Shoga kama ni mvulana au awe Msagaji kama ni msichana. Ni aibu kubwa sana kwa mpenzi wako kuwa katika makundi haya mawili na sidhani kwa akili ya kawaida kama unaweza kufurahia hiki kitu kama utakisikia au kama utakishuhudia kwa macho yako.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post