GAKI APOKELEWA KISHUJAA KITANGIRI-ANGALIA JINSI MKUTANO WA MNEC GASPAR KILEO (GAKI) ULIVYOFANYIKA KATIKA KATA YA KITANGIRI MJINI SHINYANGA

Awali mwenyekiti wa ccm kata ya Kitangiri aliyesimama bwana David Madata aliyesimama akifungua mkuatano wa hadhara tayari kwa mjumbe wa halmashauli kuu ccm taifa -NEC Gaspar Kileo (GAKI) kuwahutubia wakazi wa Kitangiri na maeneo ya jirani hapo jana

Diwani wa viti maalum CCM  kata ya kitangiri bi Marium Nyangaka akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema pamoja na kwamba kata hiyo mwaka 2010 wakati wa uchaguzi ilichukuliwa na upinzani lakini bado ccm inatekeleza ilani yake na kwamba pamoja na wapinzani kupewa nafasi ya kuongoza wananchi wameshindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kujali maslahi yao binafsi

Viongozi mbalimbali wakimsikiliza diwani wa viti maalum Marium Nyangaka akizungumza kabla ya  mgeni rasmi mheshimiwa GAKI,ambapo alisema nyumba mia tatu za wakazi wa kata ya kitangiri mkoani hapa zilizokuwa zinataka kubomolewa kupisha njia kubwa ya umeme kwenda wilayani Kahama zimezuiwa kubomolewa baada ya kubainika kuwa watu hao ni wamiliki halali wa viwanja hivyo

Wananchi wakifuatilia mkutano 

Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa(NEC) kupitia manispaa ya Shinyanga Gaspar Kileo(GAKI) akishikana mkono na kukabidhi kadi kwa wanachama wapya wa ccm zaidi ya 80 kutoka kata ya Kitangiri ambayo inaongozwa na diwani wa CHADEMA

 Zoezi la kukabidhi kadi kwa wanachama wapya  linaendelea
Wanachama wa ccm wakicheza na mgeni rasmi MNEC Gaspar Kileo GAKI katika eneo la mkutano kabla ya kuanza kuwahutubia wananchi wa Kitangiri,wanachama hao wa CCM walimvalisha kitenge kama unavyoona hapo

 MNEC GAKI akiwahutubia wananchi wa Kiatangiri mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine alisema wakati wa ziara yake katika  kata zote 17 za manispaa ya Shinyanga alizopita amekuta matatizo mengi katika kata tatu  yaani Ibadakuli,Kambarage na Kitangiri zilizochukuliwa na CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo viongozi wa upinzani badala ya kusimamia miradi ya maendeleo wamekuwa wakipinga miradi hiyo ili CCM ionekane haifanyi kazi.
Wananchi wakiwemo wanachama wa CCM na wasio wanaccm wakimsikiliza mheshimiwa GAKI ambapo GAKI alisema chama cha mapinduzi kitahakikisha kinarudisha kata ya Kitangiri mikononi mwa CCM kwani chadema imeshindwa kutatua kero za wananchi .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post