Mchungaji Daniel Kisonga akimwonyesha mbwa anayenyonyesha watoto wa Nguruwe |
Mbwa anayenyonyesha watoto wa nguruwe |
Katika hali isiyo ya kawaida
kuzoeleka ni baada ya wakazi wa Ilala katika Manispaa
ya Iringa leo kushuhudia maajabu ya dunia baada ya kushuhudia
tukio la aina yake kwa mbwa kuwachukua watoto wa
nguruwe na kuwalea kwa kuwanyonyesha maziwa yake.
Tukio hilo limetrokea machi 15 mwaka
huu majira ya asubuhi baada ya nguruwe wa mmoja kati
ya watumishi wa mungu (mchungaji ) Daniel
Kisonga kushuhudia mbwa huyo ambae alikuwa amezaa
watoto watatu na kufariki wawili na kubakia na mtoto mmoja na
hivyo kulazimika kuingia katika banda la nguruwe na kubeba
watoto wanne wa nguruwe na kuamua kuwalea na kuwapa huduma
zote ikiwemo ya kuwanyonyesha kwa upendo watoto hao wa
Nguruwe bila kuwadhuru.
Akizunguza na mwandishi wa habari
hizi leo mchangaji Kisonga amesema kuwa ni vigumu kuamini
kuna mbwa akinyonyesha watoto wa nguruwe wakati kwa
kawaida mbwa amekuwa ni mnyama hatari kwa nguruwe hao
hasa pale wanapozaliwa .
Amesema kuwa mbwawa wamekuwa wakiingia katika
mazizi ya nguruwe na kuwala nguruwe hao baada ya kuzaliwa ili imekuwa tofauti
kwa mbwa baada ya kuamua kulea watoto wa
nguruwe .
Hata hivyo amesema yawezekana ni maajabu ya dunia ila
pia yawezekana ni dalili za siku ya mwisho kama ambavyo
zimepatwa kutabiliwa katika maandiko matakatifu kuwa siku za mwisho
yatajitokeza mambo mengi ya ajabu ambayo binadamu ni vigumu kuamini mambo
hayo.
Japo upande wa
wadau mbali mbali wamehoji nguruwe hao iwapo wataendelea kunyonya
maziwa na mbwa wataliwa na binadamu ama lah ! kutokana na nyama ya
mbwa kwa kawaida kutoliwa na binadamu sasa iweje kwa
nguruwe hao kunyonya maziwa ya mbwa
Chanzo-bongonews
Post a Comment