Haijawahi kutokea Shinyanga!!!!;MAMIA YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MANISPAA YA SHINYANGA WAJITOKEZA KATIKA WARSHA ILIYOANDALIWA NA BENKI YA CRDB MJINI SHINYANGA IKILENGA KUWAFAHAMISHA KUHUSU HUDUMA NA FURSA ZA MIKOPO ZINAZOTOLEWA NA BENKI HIYO

Awali meneja wa benki ya CRDB tawi la Shinyanga bwana Said Pamui akimkaribisha mgeni rasmi bi Marium Rufunga(mke wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga),ambaye pia ni mjasiriamali katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya CRDB ikilenga kuwahamasisha wanawake wajasiriamali kutoka manispaa ya Shinyanga kuhusu huduma na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo hususani mikopo
Kushoto ni afisa wa mikopo kwa wateja wa biashara ndogo na kati kutoka makao makuu ya CRDB bi Claudina Willium akisikiliza majibu kutoka kwa meneja wa CRDB wakati akiwajibu wanawake wajasiriamali waliohudhuria warsha hiyo ambapo pamoja na mambo mengine wanawake hao zaidi ya 500 waliuliza namna ya kupata mikopo kutoka benki hiyo
Mamia ya wanawake wajasiriamali wakifuatilia mafunzo kutoka kwa afisa mikopo Claudina Willium ambaye aliwashauri wanawake wanaokatazwa na waume zao kuchukua mikopo kutoka asasi mbalimbali za kibenki waongee nao ili waweze kuwakubalia kuchukua mikopo
Wanawake wajasiriamali wakifurahia majibu mazuri ya maswali yao kutoka kwa maafisa wa CRDB,ambapo maafisa hao walisema benki hiyo ina pesa za kutosha hivyo ni kazi kwao tu kwenda kuomba mikopo
Duh! ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ulijaa kiasi kwamba wengine wakabaki mlangoni wamesimama
Katikati na mgeni rasmi Bi Marium Rufunga ,ambaye pia ni mjasiriamali akifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa ,kulshoto ni katibu wa chama cha wafanyabiashara,kilimo na viwanda Shinyanga bi Marycelina
Ukumbi ulijaa na wengine wakalazimika kukaa chini kufuatilia mafunzo hayo muhimu kwa ajili ya kujiinua kiuchimi
Mafunzo yanaendelea
Mmoja wa washiriki katika warsha hiyo maarufu kama Mama Chacha akizungumza ambapo aliwatia wanawake wenzake kuwa shupavu na jasiri hivyo wasivunike mioyo wanapokutana na changamoto wakati wa kufanya biashara zao hata wakati wa kupata mikopo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments