MCHUNGAJI ASIYEOA AISHI NA MABINTI WA WATU BILA RUHUSA YA WAZAZI WAO,ADAI ANAWAPA HUDUMA ZA KIROHO

NB-siyo kanisa na mchungaji Polite Mabesa
Na Valence Robert-Geita


Mchungaji wa  Kanisa la Emma wa Ngusu lililopo mtaa wa 14 Kambarage mjini Geita bwana  Polite Mabesa amejikuta katika kashfa ya kutorosha watoto wa kike  na kuishi nao nyumbani kwake.bila idhini ya wazazi wao kwa madai kuwa anawapatia huduma ya kiroho.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wazazi wa watoto hao  wamedai kuwa wanamshangaa mchungaji huyo ambaye bado hajaoa  kuishi na mabinti wao bila ya wao kujua kwa madai anawapa huduma ya kiroho.

Akizungumzia suala hilo balozi wa mtaa wa 14 Kambarage Sospeter Makoko  amesem aofisi yake tayari imepata taarifa za mchungaji kuishi na mabinti na kwamba anashangaa vyombo vya sheria kwanini vimekuwa bubu wakati taarifa hizo wanazo.
Aliongeza kuwa mbali na suala hilo Mchungaji huyo amekuwa kero mtaani kwao maana usiku wa manane amekuwa akipiga miziki jambo ambalo linahatarisha usalama katika mtaa huo kutokana na kelele.

Kufuatia hali hiyo  waandishi wa habari walifanikiwa kufika nyumbani kwa mchungaji huyo ili kupata ukweli,ambapo waliwakuta wasichana zaidi ya saba ambao walikuwa wakiendelea na kazi za nyumbani kwa mchungaji huyo.

 Aidha waandishi hao  walifaikiwa kumkuta mchungaji huyo na baada ya kutaka kujua ukweli mchungaji huyo alidai waandishi wamemshtukiza ilifaa wampe taarifa mapema huku akiwaomba warudi siku nyingine ofisini ili alitolee ufafanuzi suala hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post