Hatari!!!! MKAA WATEKETEZA NYUMBA WAKATI MUME NA MKE WAKIUZA MAEMBE MJINI SHINYANGA

Wakazi wa kijiji cha Ndembezi kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga wakiwa nyumbani kwa bwana Nalya Mashauri,leo Alhamis majira ya saa 5 asubuhi,wakijaribu kuzima moto ambako  umeunguza nyumba yake wakati yeye akiwa mjini Shinyanga akijitafutia mkate wa kila siku kwa kuuza maembe


Mbele ni mwenyrkiti wa kijiji hicho bwana Jumanne Maziku akishirikiana na wananzengo kuzima moto katika nyumba iliyoezekwa kwa nyasi na matete (TEMBE),moto ambao unadaiwa umetokana na mkaa uliokuwa umewekwa ndani ya nyumba hiyo na mke wa bwana Nalya Mashauri bi Happiness Philipo ambaye baada ya kuingiza mkaa huo hakubaini kama baadhi ya mikaa ilikuwa bado ina moto akafunga mlango kisha kwenda mjini kuuza maembe


Ndiyo nyumba ya Tembe iliyoungua katika kijiji hicho cha Ndembezi ndani ya manispaa ya Shinyanga


Wakazi wakiwa eneo la tukio


Gari la jeshi la  zimamoto na uokoaji mkoani Shinyanga likiwa eneo la tukio muda mchache baada ya kupewa taarifa kuwa kuna tukio la nyumba kuungua


Miongoni mwa vitu viliyokuwa ndani ya nyumba hiyo,vingine ni nguo,vitanda,vyombo,makochi n.k vilivyoteketea kwa moto ingawa jumla ya thamani yake haikueweza kujulikana mara moja


Maafisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji wakizima moto huo ingawa pamoja na jitihada zote hizo moto huo ulikuwa umeteketeza mali nyingi


Shughuli ya kuzima moto inaendelea


Maembe yakiwa ndani ya nyumba iliyoteketea kwa moto unaodaiwa kusababishwa na mkaa uliokuwa ndani ya nyumba hiyo



Kulia ni Station Sajenti Peter Kindimani kutoka jeshi la zimamoto mkoa wa Shinyanga ,aliyeongoza zoezi  la kuzima moto huo akizungumza na mwenyekiti wa kijiji cha Ndembezi Jumanne Maziku(mwenye shati la kitenge) ambapo alitoa rai kwa viongozi wa maeneo mbali mbali kuwashauri wananchi kujenga tabia ya kutoa taarifa kwa njia ya simu kwa jeshi hilo pindi tu matukio kama hayo yanapojitokeza ili waweze kufika kwa wakati kwa ajili ya kuzima moto na kuokoa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post