WATENDAJI WAMCHEFUA DIWANI !! NI WALE WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA WANAOKWEPA MAJUKUMU YAO KAMA VILE KUKWEPA KUSOMA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI KWA WANANCHI

Kushoto ni diwani wa Kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga,ambaye pia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Mheshimiwa David Nkulila akizungumza katika kikao cha kamati ya maendeleo ya kata hiyo ambapo aliwataka baadhi ya watendaji wa vijiji na kata katika manispaa hiyo kuacha kukwepa majukumu yao ikiwemo kukwepa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi kwa madai kuwa hiyo ni kazi ya wenyeviti wa vijiji na au mitaa.Kulia ni afisa matendaji wa kata hiyo James Dogani akiandika mawili matatu katika kikao hicho

Afisa afya wa kata ya Ndembezi bwana Sanya Anthony Mwara akisoma taarifa kuhusu idara yake 

Mwenyekiti wa kijiji cha Ndembezi bwana Jumanne Maziku akizungumza katika kikao hicho

Mratibu wa elimu kata ya Ndembezi bwana Suleiman Burugu wakati wa kikao hicho amabpo alisema kata yake inakabiliwa na changamoto ya wanafunzi wengi kutojua kusoma,kuandika na kuhesabu hasa shule ya msingi Ndembezi

 Kushoto ni mwenyekiti wa mtaa wa Mbuyuni katika kata ya Ndembezi bwana Chifu Abdallah Sube akiandika mawili matatu katika kikao hicho kama vile suala la wafanyabiashara katika mtaa huo kuongoza kwa kukata leseni za biashara zao
Kushoto ni mwandishi wa gazeti la Nipashe bwana Marco Maduhu,katikati ni bi Veronica Helya ambaye ni Program Organiser kutoka shirika lisilo la kiserikali la BRAC lenye lenye lengo la  kuwawezesha wananchi hususani watoto wa kike katika suala zima la elimu pamoja na kuongeza mahudhurio ya wanafunzi wa kike mashuleni kuanzia darasa la 5,6 na saba lakini pia kidato cha kwanza na pili,kushoto ni bi Grace Chandika ambaye pia ni program organiser kutoka BRAC wakifuatilia kikao hicho hapo jana

Bi Grace Chandika akitambulisha shirika lake la BRAC kwa viongozi wa kata ya Ndembezi ambapo alisema lengo lao kuwawezesha watoto wa kike katika suala la elimu na pia wanaangalia sana watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu na wataanza shughuli nzima mwaka ujao 

Wa kwanza kulia ni bwana Kadama Malunde,mwandishi wa habari Gazeti la Zanzibarleo na Radio Kahama pia mkurugenzi wa www.malunde1.blogspot.com akiwa katika kikao hicho

 Katika kikao hicho kilicholenga kujadili maendeleo ya Kata hiyo,Wajumbe wa kikao hicho walisema kata yao ina Radio,ambapo Diwani wa kata ya Ndembezi/Naibu Meya manispaa ya Shinyanga David Nkulila aliuomba uongozi wa Radio Faraja fm Stereo inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo la Shinyanga kuona umuhimu wa Kutumia kata ya Ndembezi wanapojitambulisha/tangaza. MFANO BADALA YA KUSEMA WAKITANGAZA KUTOKA NGOKOLO BASI WASEME WAKITANGAZA KUTOKA NDEMBEZI kwani radio hiyo iko katika Kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post