UTAPELI GEITA---!!! ZAIDI YA MAWAKALA 1200 WA VODACOM MPESA MKOA MZIMA WA GEITA WAPATIWA MAFUNZO KUKABILI UTAPELI ULIOENEA MKOANI HUMO
Na Valence Robert, Geita.

Zaidi ya mawakala 1200  wa Vodacom m-pesa kutoka  mkoa wa Geita wamepewa mafunzo  kuhusu jinsi ya kuwahudumia wateja wao pamoja na mbinu za   kuepukana na matapeli waliotapaa  katika mkoa mzima wa Geita wanaojitambulisha kuwa wao ni wafanyakazi kutoka kampuni ya Vodacom.
Akizungumza katika semina hiyo ya siku moja  iliyofanyika jana katika ukumbi wa Bwalo la polisi mkoa wa Geita mwezeshaji wa mafunzo hayo bwana  Biseco kutoka makao makuu ya kampuni ya Vodacom jijini Dar es salaam amesema lengo kubwa la mafunzo hayo  ni kuwafundisha mawakala hao kuhusu namna ya  kuhudumia wateja na kuepukana na matapeli wanaojitokeza.
Bwana  Biseco amesema  kuna matapeli wanaotapeli watu kwa kutumia jina la  mpesa huku wakijitambulisha kuwa wao ni  wafanyakazi wa kampuni ya vodacom wakati sio kweli na hivyo kuwatapeli  mawakala hao.
Amewataka  mawakala kuacha  kununua laini za [ TILL]  mitaani na kwa wale mawakala wanaouza [TILL] wakibainika watapelekwa mahakamani  kujibu mashitaka yatakayowakabili.
Naye meneja masoko  mkoa wa Geita Julius Peter amewataka mawakala na wateja wote wa mkoa Geita kuwa makini wanapopewa huduma na kutoa huduma kwani matapeli wamekuwa wengi sana katika mkoa mzima wa Geita na wawaepuke matapeli hao.
Kwa upande wao mawakala kutoka wilaya tano za mkoa mzima wa Geita ambazo. ni Geita, Chato, Mbogwe, Bukombe na Nyagware wameshukuru sana kampuni ya Vodacom kwa kutoa mafunzo hayo  na kuahidi kutoa huduma kwa uangalifu na umakini zaidi ikiwa ni pamoja na  kuepukana na matapeli waliotapakaa mkoa mzima wa Geita kwa kujiita watumishi wa vodacom m –pesa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post