MTU MWINGINE AFUFUKA ,AONEKANA AKITEMBEA BARABARANI MCHANA KWEUPEEEEE


NB haya ni makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga

Na Valence Robert,Geita
Siku chache tu baada ya mtoto kudaiwa kufufuka hofu  imezidi kutanda miongoni mwa wakazi wa mkoa wa Geita,ambapo  mtu mwingine anayedaiwa kufariki dunia zaidi ya mwaka mmoja uliopita kuonekana akiwa hai huko katika kijiji cha Rumasa kata ya Buseresere wilaya ya Chato mkoani Geita.
Mtu huyo anayefahamika  kwa jina la Mgonda Thomas (22) ambaye anasemekena kuwa alifariki dunia Mei 28,mwaka jana,ameonakana akiwa hai juzi majira ya saa 9 alasiri wakati akitembea barabarani jirani na nyumbani kwao.
Imeelezwa kuwa majirani walipomuona walimtambua kwa sura mtu huyo  na  baadaye waliamua kutoa taarifa kwa ndugu zake wakiwemo wazazi wake ambao ni Thomas Msalaba (60) na Martha Kitobelo ambapo walipomuona nao walimtambua kwa sura na alama ya kovu la mkono wa kushoto lilitokana na kuungua kwa moto wakati wa uhai wake.
Kufuatia tukio hilo la kushangaza ndugu zake walimchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji Juma Tabiho umbali wa kilomita moja kutoka nyumbani kwao kutokana na kulihusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Hata hivyo jeshi la polisi wilayani Chato likiongozwa mkuu wake wa wilayani humo, Leonard Nyaoga lililazimika kufanya kazi ya ziada kuwatuliza wananchi waliotaka kufukua kaburi kujua kilichomo ambapo baadaye askari walimchukua na kumpeleka kituoni kwa maojiano zaidi.
Tukio hilo limetokea ikiwa ni wiki mbili baada ya mtoto Shaaban Maulidi(16)aliyefariki dunia mwaka 2011 kuonekana akiwa hai septemba 28,mwaka huu katika Mtaa wa 14 Kambarage mjini Geita.   

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments