KIKONGWE AFUNGUKA KUHUSU NYUMBA ILIYOUZWA HUKU WATOTO WAKIWA NDANI -MBEYA

 
 
Mariamu Mponzi mwenye miaka  kati ya  80- 85 ambaye ndiye mama mzazi na Emmanuel Yuta muuzaji wa nyumba ametoa yake ya  moyoni baada ya kufanikiwa kuikomboa nyumba kutoka kwa mnunuaji




  
Mama huyo aliyejulikana kwa jina la Mariamu Mponzi anakadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 80 na 85 ambaye ndiye mama mzazi na Emmanuel Yuta muuzaji wa nyumba hiyo ametoa ya moyoni baada ya kufanikiwa kuikomboa nyumba kutoka kwa mnunuaji.

Kikongwe hiyo alichukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa kitendo kilichofanywa na mwanae akishirikiana na serikali ya kijiji si cha kiungwana cha kuuza nyumba ya familia na kuwaacha watoto wasijue la kufanya.

Aidha alilazimika kukopa fedha toka kwa majirani jumla ya shilingi 410,000/= ambazo mnunuzi Dati Nsagaje alidai arudishiwe ili naye aachie nyumba hiyo jambo ambalo bibi huyo alifanikiwa, hata hivyo nyumba mbili pamoja na uwanja viliuzwa kwa jumla ya shilingi 750,000 na mnunuaji alitoa kianzio cha shilingi 400,000/= na shilingi 10,000/= alidai ni usumbufu alioupata.

Akizungumza baada ya kurejesha nyumba hiyo kikongwe huyo alisema kwa sasa nyumba hiyo ni mali ya wajukuu zake hivyo mwanae akishindwa kuendelea na maisha alikokimbilia na kuamua kurejea nyumbani asikanyage katika nyumba hizo bali akatafute mahali pengine pa kuishi.

Alisema inaweza ikamfikia taarifa kuwa nyumba imerudishwa hivyo hapa hatatakiwa kukanyaga kwa sababu hiyo ni mali ya wajukuu zake na yeye itambidi kutafuta eneo lingine na kuanza upya kujenga.

Mkasa huo wa ajabu ulitokea katika kijiji cha Hatwelo, Kata ya Ijombe Mbeya Vijijini ambapo Mkazi huyo aliyefahamika kwa jina la Emmanuel Yuta alipouza nyumba yake na kutokomea yeye na mkewe na kuwaacha watoto wawili wenye umri kati ya miaka 9 na 11 wakikosa mahala pa kuishi.

Kutokana na kitendo hicho kutokubalika, baadhi ya Majirani  walisema ni kitendo cha kinyama na hakipaswi kufumbiwa macho ambapo waliamkopesha fedha ili kuikomboa nyumba ili irudi mikononi mwa watoto.

Baada ya kupata fedha hizo, Kikongwe huyo alitoa shilingi 410,000/= alizokuwa amedai mnunuaji ili aweze kurejesha nyumba ikiwa ni fedha alizokuwa ametoa awali hivyo kukubaliana kuicha nyumba hiyo ambayo kwa mujibu wa majirani na baadhi ya ndugu wamesema itakuwa ni mali ya watoto.

Alisema hadi sasa amefanikiwa kurudisha fedha kiasi kwa waliomkopesha na bado anadaiwa shilingi 100,000/= anazotegemea kurudisha baada ya kuuza viazi anavyolima yeye mwenyewe kutokana na hali ya mumewe kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya magonjwa na uzee.

Aidha juhudi za bibi huyo kuikomboa nyumba hiyo na kuwa mali ya watoto zilifanikiwa ambapo mnunuzi Datistani Mwanshinga alibatilisha ununuzi wa nyumba hiyo Mei 9, Mwaka huu baada ya kukiri kurejeshewa fedha zake.
CHANZO-MBEYA YETU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments