MAJANGA MENGINE--!! MUME ANYONGA MKE KITANDANI HUKU YEYE AKIJINYONGA KWA KAMBA YA KATANI-KISHAPU


Mwanamke aliyejulikana kwa jina laVeronica Stephano (25) mkazi wa kijiji cha Idukilo kata ya Mwadui wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ameuawa kunyongwa na mme wake aitwaye Salawa Nhela(35)  na baada ya kumuua mke wake naye akajinyonga.
  
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Evarist Mangalla amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa moja asubuhi ambapo mwanamke huyo amekutwa amefariki dunia  kitandani baada ya kunyongwa na mume wake na baada ya mwanamme huyo kufanya tukio hilo naye aliamua kujinyonga  kwa kutumia kamba ya katani juu ya dali ndani ya chumba chao.

Amesema chanzo cha tukio hilo  inadaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi kufuatia mwanamme kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine na kuongeza kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments