BALOZI WA CHINA NCHINI LU YOUQING AUNGANA NA KATIBU MKUU CCM TAIFA ABDULRAHMAN KINANA KATIKA ZIARA YAKE WILAYANI KISHAPU
Viongozi wa CCM wakiriki kuchekecha mchanga kwa ajili ya ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya Sekondari Mwigumbi.Kulia ni ndugu Kinana kushoto ni mbunge wa Kishapu S.Nchambi,aliyeshika koleo ni ndugu Nape Nnauye


Mwenyekiti wa CCM Hamis Mgeja akiwasalimia na kuwaomba kuendelea kuipenda CCM wakazi wa Kijiji cha Mwigumbi wilayani KISHAPU


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hillal akizungumza katika eneo la mradi wa kisima kirefu cha maji Mwigumbi ambapo aliiomba serikali kufikisha mradi wa maji ya Ziwa Victoria ufike pia Kishapu

Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akitaja mafanikio waliyofikia katika jimbo hilo kuwa ni kutoa huduma ya chakula mashuleni,umeme,huduma za afya,barabara na maji


Ndivyo ilivyokuwa katika mkutano wa hadhara katika eneo la mnada Mhunze wilayani Kishapu


Kulia ni balozi wa China hapa nchini Lu Youqing akizungumza katika mkutano wa hadhara eneo mnada Mhunze Kishapu ambapo alisema Wawekezaji kutoka China tayari wapo Shinyanga kwa ajili ya viwanda mbalimbali vikiwemo vya pamba.Katikati ni Ndugu Kinana na kushoto ni Katibu wa itikadi na uenezi Ccm taifa Nape Nnauye akitafsiri kile alichokuwa anazungumza Balozi wa China kwa wananchi(Balozi Kiingereza na Kichina,Nape Kiswahili na Kisukuma)


Kulia ni mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akimwonesha kwa vitendo Balozi wa China hapa nchini bwana Lu Youqing(katikati) namna ya kucheza ngoma ya jeshi la jadi Sungusungu.Kulia ni ndugu Abdulrahman KinanaMoja kati ya majengo ya Hospitali ya wilaya ya Kishapu inayoendelea kujengwa ili kuwasogezea huduma ya afya wananchi badala ya kusafiri umbali kwenda shinyanga mjini iliko Hospitali ya mkoa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments