Wanachama wa CCM wakifuatilia hotuba ya mwanyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Shinyanga
ndugu Hamis Mgeja amewataka wananchi
kuacha kubeza mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya CCM tangu iingie madarakani mwaka 2010, na kuongeza
kuwa hakuna serikali yoyote duniani isiyokuwa na matataizo na njia pekee ya
kuondoa matatizo ni kufanya kazi kwa juhudi na maarifa wala siyo kukikimbia
chama.
Mgeja ameyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika
katika eneo la Ngokolo Mitumbani Mjini Shinyanga wakati wa ziara yake kuangalia
utekelezaji wa ilani ya CCM tangu iingie
madarakani mwaka 2010 ambapo alisema mambo kadha wa kadha yamefanywa na chama
hicho ikiwemo masuala ya elimu,barabara,maji na
afya na kutoyaona mafanikio yaliyofikiwa akalinganisha na shukrani ya punda kuwa ni mateke.
Amesema mkoa wa Shinyanga hivi sasa una mabadiliko makubwa
kwani wananchi wanapata maji safi na salama
kutoka ziwa Victoria
huku viwanda mbalimbali vikiendelea kujengwa hali ambayo itasaidia vijana wengi
kupata ajira.
Aidha amewataka wananchi kuwapuuza wapinzani wanaohubiri
kuhusu maandamano ama nguvu ya umma na kusisitiza kuwa hakuna serikali yoyote
duniani iliyoingia kwa njia ya nguvu ya umma imefanikiwa.
Post a Comment