Imeelezwa kuwa walimu katika
shule ya msingi Mwenge iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wanatumia wanafunzi
wao kusahihisha mitihani ya wanafunzi
wenzao hali ambayo imetajwa kuchangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika
shule hiyo.
Wakizunguza katika kikao cha wazazi na walezi
wa wanafunzi kilichoenda sambamba na kufunga shule hiyo kilichofanyika katika shule
hiyo mjini Shinyanga wazazi na walezi hao wameeleza kukerwa na tabia
iliyoanzishwa na walimu kutumia wanafunzi kusahihisha mitihani ya wanafunzi
wenzao hali inayohatarisha ufaulu wa wanafunzi hao kwani hakuna umakini wowote
katika usahihishaji huo ambapo penye kosa huwekwa vema.
Akizungumzia kuhusu suala
hilo mgeni rasmi , ambaye ni Katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga bwana
Boniface Chambi alisema walimu katika shule ya msingi Mwenge hawafanyi maksudi
bali tatizo hilo linatokana na idadi ndogo ya walimu ukilinganisha na idadi ya
walimu waliopo shuleni hapo.
Amesema Katika shule hii kuna walimu
21 pekee wakati wanafunzi wako 1200,hivyo walimu wanalazimika kutumia wanafunzi
wenye uwezo mkubwa darasani wa madarasa ya juu ili kuwasaidia wadogo zao
Naye mwalimu mkuu wa shule
hiyo bwana Mahamudu Ibrahim amesema suala hilo linajitokeza zaidi wakati wa
mitihani kwa ajili ya kuandaa haraka matokeo pindi shule inapofungwa tatizo
linalochangiwa na uhaba wa walimu shuleni hapo.
Hata hivyo mwalimu huyo mkuu amesema ili
kuhakikisha matokeo kwa wanafunzi wake yanakuwa mazuri,walimu katika shule hiyo
wanalazimika kufundisha kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni badala ya kuishia saa
8 :30 mchana kama inavyotakiwa.
Kwa upande wao wazazi na
walezi wa wanafunzi waliohudhuria kikao hicho wameiomba serikali kuiangalia kwa
jicho la huruma shule hiyo kwa kuongeza walimu wa kutosha kwani ni aibu kubwa
sana kwa wanafunzi kusahihisha mitihani ya wanafunzi wenzao na kitendo hicho
inapelekea kushuka kwa kiwango cha elimu hapa nchini.
Post a Comment