HATARI: AJINYONGA BAADA YA KUNYIMWA TENDO LA NDOA NA MKEWE
Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Mkazi
wa mtaa wa Mpanda hotel wilaya yam panda mkoa wa katavi Nzego Vicent
(33) amejiua kwa kujinyonga na kamba baada ya mkewe kumnyima tendo la
ndoa.
Tukio hilo limetokea hapo juzi majira ya saa 7:30 usiku jirani na nyumba waliokuwa wakiishi wanandoa hao.
Mke
wa marehemu huyo aitwaye Agnes Nicodemu alisema siku hiyo ya tukio hilo
mumewe ambaye alikuwa ametoka kwenye pombe za kienyeji alifika nyumbani
kwake majira ya saa 6:20 usiku na kumtaka mkewe ampe tendo la ndoa.
Alisema
kutokana na shughuli alizokuwa amezifanya mchana alimwomba mumewe
avumilie hadi siku itakayofuata kwa kile alichomweleza kuwa hakuwa
tayari kufanya nae tendo landoa kwa kuwa alikuwa amechoka.
Baada
ya marehemu Nzego kujibiwa hivyo hakuridhika nna kauli hiyo ya mkewe na
ndipo alipoanza kumshutumu kuwa huenda ana mahusiano ya kimapenzi na
wanaume wengine.
Ndipo
Nzego alipoamua kuanza kumshambulia mkewe huyo kwa kumpiga kichapo huku
akimtolea maneno ya kumtisha kuwa lazima atamuua kwa panga.
Agnes baada ya kuona kipigo kimezidi aliamua kukimbia nje ili kukwepa kipigo alicho kuwa akichapwa na mumewe.
Baada
ya mkewe kukimbia marehemu aliamua kutoka nje huku akiwa na shoka mbili
na kuelekea kusiko julikana na kuacha nyumba yake ikiwa wazi.
Ndipo
majira ya ssa 12:30 asubuhi mkewe na marehemu alipofuatwa na majirani
na walimweleza kuwa mumewe amejinyonga kwa katani jirani na nyumba
waliyokuwa wakiishi.
Mkewe
huyo aliamua kufuatana na majirani hao hadi kwenye eneo hilo na ndipo
alipomwona mumewe akiwa amening’inia juu ya mti akiwa amekata roho.
Kamanda
wa polisi mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa
kifo hicho cha mtu kujinyonga kwa kutumia kamba katika mtaa huo
Social Plugin