Mwandishi Auawa Syria

Mwandishi wa Syria na mtafiti wa kisiasa, aliyejulikana kwa maandisi yake makali ya kuchochea kupinga Uyahudi, ameuwawa kwa kuteswa na usalama wa taifa wa Syria.

Taarifa ya kifo hicho ni kwa mujibu wa familia yake na vikundi vya upinzani. Mohammed Nimr al-Madani, aliyekuwa na umri wa miaka 51, aliuwawa siku 10 zilizopita lakini mpaka sasa mwili wake bado upo katika mikono ya maafisa wa ujasusi wa Syria.

Mwandishi huyo aliyekuwa baba wa watoto watatu aliwahi kukamatwa mara tatu na maafisa usalama wa taifa tangu kuanza kwa vuguvugu la mageuzi la kumpinga Rais Bashar al-Assad Machi 2011.

Makundi ya wanaharakati wanasema Nimr alikuwa mwakilishi wa siri wa vyombo vya habari vya kigeni nchini humo.

Katika ukurasa wake wa facebook marehemu amejielezea kuwa ni mtaalamu wa masuala ya dini na maangamizi ya Wayahudi, tukio ambalo amelikanusha vikali katika maisha yake yote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments