Kwa wale walioondoka mapema kwenye show ya Fiesta usiku wa kuamkia Jumapili baada tu ya Rick Ross kumaliza performance yake, walikosa kujionea kituko kilichofanywa na Diamond Platnumz. Ama wengine wamekuja tu kuona picha zilizosambaa kwenye internet
Akiwa stage na madancer wake wakati show imepamba moto, Diamond aliamua kuvua na kuonesha boxer yake nyeupe kama ishara kuwa yeye na madansa wake ni ‘wasafi’ kiasi cha kutoogopa kuionesha hadharani.
Bahati mbaya watanzania wamemuelewa tofauti. Kitendo hicho kimewakera wengi.
Kwa mujibu wa maoni tuliyoyapata kupitia ukurasa wetu wa Facebook baada ya jana kuweka picha hiyo, wengi wameitafsiri picha hiyo kama ishara ya ‘ushoga’ na huku wengine wakienda mbali zaidi na kuibua tena mada ya ufreemason. Haya ni baadhi ya maoni.
“Wanaonyesha kuwa na mapepo hao maana walianza na kuvua magoti hadi
mashati wakabakiza suruali , sasa wamebakiza boxer unadhani wakishatoa
boxer watabakiza nini, huo ni ushirikina na muda si mrefu watahumbuka
hao maana naona ule mwisho wao umeshafika; hizo ni akili ama matope…wana
akili ama matahairaaaaa1.”
“Ndio maana wazee wetu hawaupend kuusikiliza huu muzk munaoita bongo
flava. Uchafu kama huu mnafanya mbele za watu au umaarufu unatafutwa kwa
kila njia,basi huyo tanzanite awe john elton wa bongo.”
“Lbd alielewa tofauti,alpockia MUONEKANO MPYA BURUDAN ILEILE ndani ya
fiesta!!nd mana akafanya hcho k2ko lkn pia mayb woz search and luking
fo huzband! nadhan co rdhk nyota uyu.teh teh teh shame upon hiz
unimpressive kboxa.”
“Huu ni upuuzi wa wasanii wetu. Yaani huyu ndiye anayeitwa staa
ambaye hana hata chembe ya adabu?? Na ninyi mnaangalia tu
mnamshangilia???”
“OH! Lord hav marcy on this young man.This is devilish coz there s no any gud motivation to build up our society.Kwanini wasanii wa africa wanapenda kuiga utamaduni wa wa zungu? ambao haujengi jamii ye2 bali ina teketeza.kama we ni muimbaji kuja na stail ya utamaduni wako dnt promote someones cultur,mbona wao hawapromot utamaduni wenu,b yoself dnt try b somebody else,the moment u try to imitate frm someone u ll mess up coz u ll never b that person.U were created as a unique person so b u.”
“Nampenda diamond lakn kwa mambo haya mmh…. hapana kwakweli, sa
kulikua na haja gani ya kupanda jukwaan na nguo ta2 c wangeziacha2 home
wakaingia na hivo vchup au ndo vilikua vpya!!”
“What are they doing???/ is Diamond Freemasons..coz what they are
doing is inhuman..i don’t know that what am thinking..if dancing is like
that then we don’t have to…are u feeling happy watching something like
this…damn Diamond.”
“Soko la entertainment tz linagonga mlango wa shetani…bado mtayaona ya laana zaidi ili wafanikiwe..ni huruma sana coz hao waliotangulia kuingiza soko lao la burudani mikononi mwa shetani wanajuta na 2nashuhudia wanavyoendeshwa na wengine wakituonya kwa bidii,ila wabongo ndo wanakimbilia huko..they’ll sell their soul for money and fame..watch out fo that!”