Wakili Allute Lissu Mughwai ambaye ni kaka wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amefariki usiku wa kuamkia Leo Novemba 1, 2026.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dada yake aitwaye Rose Masesa pindi alipozungumza na Jambo TV.
Jambo TV ilipotaka kufahamu chanzo cha kifo chake Rose ametueleza kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza lolote huku akitueleza kuwa msiba upo jijini Arusha.
"Ni taarifa za kweli msiba upo Arusha na mimi naelekea huko" alisema Rose kwa ufupi.
Mkurugenzi wa Habari, Mawasiliano na Uenezi wa Chama hicho, Brenda Rupia amethibitisha kutokea kwa msiba huu, amesema "Ni taarifa ya kweli, msiba umetokea na sasa viongozi wetu wanaelekea gerezani kuonana na Mwenyekiti baada ya hapo tutatoa taarifa rasmi na kamili
TAFUTA HABARI
Kamusi
Social Plugin