Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUFUNGUA MILANGO KWA WAWEKEZAJI BINAFSI BANDARI YA NYAMIREMBE GEITA



Na Mwandishi wetu, Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, amesema Serikali itachunguza uwezekano wa kuruhusu wawekezaji binafsi kuingiza meli zao katika Bandari ya Nyamirembe wilayani Chato mkoani Geita hatua ambayo inalenga kuanzisha tena huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo ili wananchi wanufaike na uwekezaji uliofanywa

Amesema hayo wakati wa ziara ya kutembelea bandari hiyo tarehe 17 Novemba 2026 mkoani humo na kueleza kuwa Wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) itashughulikia changamoto zilizopo ikiwemo kuchunguza kina cha maji na ufanisi wa kibiashara ili kubaini ukubwa wa meli zinazoweza kutumia bandari hiyo ambayo imejengwa kwa zaidi ya Shilingi bil.6

Aidha Kihenzile ameitaka TPA kuangalia namna ya kuwapa fursa za ajira vijana wa eneo hilo zinahusisha upakiaji na upakuaji wa mizigo na kusisitiza kuwa uwekezaji wa Serikali unapaswa kuwanufaisha wananchi katika maeneo yao kwa kuongeza ajira na shughuli za kiuchumi ikiwa ninutekelezaji wa Dira 2050

Akizungumzia usalama wa usafiri wa maji amesema Serikali kwa kushirikiana na Kenya na Uganda imejenga vituo vitatu vya utafutaji na uokoaji katika maeneo ya Ilemela, Kanyara na Bunda. Pia inaendelea kujenga na kukarabati meli, ikiwemo MV Mwanza na meli nyingine yenye uwezo wa kubeba tani 3,000, imeshanunua boti za uokozi Hatua ambazo zinalenga kuimarisha usafiri na usalama katika Ziwa Victoria

Kwa upande wake Mbunge wa Chato Kaskazini Mhe. Cornel Magembe ameiomba Serikali kuhakikisha bandari hiyo inaanza kutoa huduma kikamilifu na uogeza kuwa itarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka Dar es Salaam kupitia Mwanza na kuimarisha biashara na Rwanda, Burundi na DRC

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Maiko Kachoma, amesema wananchi wanakabiliwa na changamoto za usafiri wa majini hususan huduma za vivuko. Ameeleza kuwa ajali ya kivuko iliyowahi kutokea ilihusisha abiria 127 ambapo 102 walipoteza maisha na kuiomba Serikali kuimarisha huduma za meli pamoja na kuweka kituo cha utafutaji na uokozi.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com