Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUCHUNGUZA CHANZO CHA HITILAFU YA MELI MWANZA




Na Mwandishi wetu, Mwanza

MKuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Salum Hamduni amewahakikishia wananchi kuwa meli iliyopata hitilafu wakati wa majaribio ya maandalizi ya kuanza safari zake iko salama huku Serikali ikipanga kufanya uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tukio hilo

 Hamduni amesema tathmini ya awali iliyofanywa na wataalamu imeonesha kuwa meli hiyo iko salama huku Serikali ikiamua kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini sababu halisi ya tukio hilo na madhara yaliyoweza kujitokeza

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 18 Nov, 2026 Jijini Mwanza Mhe. Hamduni amesema meli hiyo ilikuwa imekaa kwa muda mrefu bila kufanya safari huku Serikali kupitia Kampuni ya meli Tanzania (TASHICO) ikiendelea na maandalizi ya kurejesha huduma zake kwa kuzingatia ratiba zilizopangwa

“ Niwahakikishie wananchi kuwa kwa mujibu wa uchunguzi wa awali uliofanywa na wataalamu wetu meli yetu iko salama hivyo tunataka kujihakikishia usalama zaidi kwa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha tukio hili,” amesema Mhe. Hamduni."

Aidha Serikali ya Mkoa imewasiliana na Wizara ya Uchukuzi na kutoa maelekezo ya Serikali kuwa timu ya wataalamu itaundwa kwa kushirikiana na wizara husika, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na mamlaka nyingine za Serikali ili kufanya uchunguzi huo

Vilevile amesisitiza kuwa taarifa anazozitoa ndizo taarifa rasmi za Serikali ya Mkoa huku akiwataka wananchi kuepuka kusambaza taarifa zisizothibitishwa zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com