Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC MTANDA AKABIDHI CHETI CHA USAJILI TACOEJ, AAHIDI USHIRIKIANO


MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha Usajili kwa waandishi wa Habari za Pamba na Mazingira (TACOEJ), kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TACOEJ, Costantine Mathias, kulia ni Mary Joseph (Mjumbe) na Sitta Tuma (wa pili kulia) ambaye ni Katibu Mtendaji.

‎Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.

MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Said Mtanda amekabidhi rasmi cheti cha Usajili wa Chama cha Waandishi wa Habari za Pamba na Mazingira (Tanzania Cotton and Environmental Journalists-TACOEJ) kilichotolewa na serikali huku akiwaahidi ushirikiano katika kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishaji wa pamba.

‎Mtanda amekabidhi cheti hicho, leo Novemba 03, 2026 ofisini kwake mara baada ya kutembelewa na viongozi hao na kuwaahidi ushirikiano katika kuhamasisha wakulima kulima kilimo chenye tija.

‎Amesema kuwa atahakikisha anajifunza kwa haraka kuhusu Kilimo cha Pamba na kwamba atashirikiana na waandishi wa habari za pamba kuhamasisha wakulima wa pamba kuongeza tija ili kukuza Uchumi wa wakulima wa pamba.
‎
‎"Pamba ni uti wa mgongo (backbone) wa Uchumi wa Mkoa wa Simiyu, zao hili lina changamoto nyingi sana na mimi kama mkuu wa Mkoa ninatakiwa kujifunza haraka nijue changamoto za zao la pamba." Amesema na kuongeza.

‎"Na tumekubaliana, pia tunayo maagizo ya serikali kufanya vikao vya wadau kabla, ninyi mnataka kufanya kongamano, mimi naona ni tofauti...ninyi tunatakiwa tushirikiane na Mamlaka zetu kuandaa kikao cha wadau Kwa ajili ya zao la pamba na ninyi mtatumia kalamu zenu kiuandishi kufikisha ujumbe mkiwa ni sehemu ya wadau wa Pamba ili yale tuliyokubaliana tuyatolee Elimu kwa umma".

‎Amesema kuwa watahakikisha wanahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji wa pamba ili waweze kutoka kuzalisha tani 133,000 na kufikia uzalishaji wa tani 200,000... hivyo ni lazima kufanya jitihada Kwa kushirikiana na waandishi wa habari za Pamba na Mazingira ili jamii na umma ujue Pamba ni kitu gani na Uchumi wa Simiyu unategemea zao la pamba.‎
Ameongeza kuwa atahakikisha wanashirikiana na wadau wengine wa sekta ndogo ya Pamba na mazingira kwa kukutana mara kwa maa na kuweza kuchukua changamoto za pamba ili ziweze kutatuliwa kwa wakati.

‎Awali Katibu wa TACOEJ, Sitta Tumma amesema kuwa watatumia taaluma yao ya Uandishi wa Habari kuhakikisha Elimu sahihi ya Kilimo cha Pamba inawafikia wakulima ili waongeze tija katika uzalishaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com