Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KISHINDO CHA SAMUU PRIMARY SCHOOL NECTA 2026! WANAFUNZI WOTE 75 WAPATA DARAJA A

Ni furaha na mafanikio makubwa katika safari ya elimu! Shule ya Msingi SAMUU iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga imeweka alama ya kipekee katika Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) mwaka 2026, baada ya wanafunzi wake wote 75 waliofanya mtihani huo kupata Daraja A, sawa na asilimia 100 ya ufaulu.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), shule hiyo yenye namba PS1704058 imepata wastani wa alama 284.6800 na Daraja A (Bora).

Kati ya wanafunzi hao, wavulana 43 na wasichana 32 wote wamepata Daraja A, bila kuwa na mwanafunzi aliyepata daraja B, C, D au E.

Katika ufaulu wa masomo, English Language imeongoza kwa wastani wa alama 49.6800 kati ya 50, ikifuatiwa na Sayansi na Teknolojia (49.0400), Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi (48.1067), Hisabati (47.6000), Uraia na Maadili (45.8267) na Kiswahili (44.4267).

Mafanikio hayo ni kielelezo cha juhudi za walimu, wanafunzi, wazazi na uongozi wa shule katika kuimarisha ubora wa elimu.

Hongereni wanafunzi wote 75, walimu na wazazi kwa mafanikio haya makubwa!

Breaking : TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA 2026

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com