Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA APIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO



Na Dotto Kwilasa, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepiga kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino, uliofanyika leo Novemba 4, 2026, katika Kituo cha Kupigia Kura cha Ofisi ya Kijiji cha Chamwino mkoani Dodoma.

Rais Samia ameshiriki katika zoezi hilo la uchaguzi kwa kupiga kura katika kituo hicho, ambacho ni miongoni mwa vituo vilivyotumika katika uchaguzi mdogo wa kuwapata mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Chamwino.

Uchaguzi huo umefanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Mhe. Deogratius Ndejembi, kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatua iliyoacha nafasi ya ubunge wa jimbo hilo wazi na kuhitaji uchaguzi mdogo ili kupata mwakilishi mpya.

Ushiriki wa Rais katika zoezi hilo unaonesha nafasi ya wananchi katika kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka kuwasimamia na kuwawakilisha katika vyombo vya maamuzi.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com