Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

LIMBE ATANGAZA MILIONI 50 KUCHIMBA KISIMA KIREFU MWALATA -KISHAPU


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Josephat Limbe, akizungumza na wananchi katika mkutano wake wa hadhara wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Kijiji cha Mwalata, Kata ya Ndoleleji, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Novemba 3, 2026


Na Sumai Salum-Kishapu


Wananchi wa Kijiji cha Mwalata, Kata ya Ndoleleji, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, wameiomba Serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama, wakieleza kuwa wanalazimika kutembea umbali wa takribani zaidi ya kilometa sita kufuata maji katika Mto Tungu, hali inayowaweka katika mazingira hatarishi na kuwaathiri kiuchumi na kijamii.


Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Josephat Limbe uliofanyika Novemba 3, 2026, katika Kitongoji cha Matundulu, wananchi hao wamesema muda mwingi wanautumia kutafuta maji badala ya kushiriki shughuli za uzalishaji mali na shughuli nyingine za maendeleo.


Mkazi wa kijiji hicho, Gaudencia Jisandu, amesema changamoto hiyo imekuwa mzigo mkubwa kwa wanawake na familia kwa ujumla, huku akiiomba Halmashaur kuwasaidia kuharakisha upatikanaji wa huduma hiyo., "Wanawake hulazimika kuamka mapema na kutembea umbali mrefu kutafuta maji, hali inayowaathiri katika shughuli za kiuchumi na ustawi wa familia" amesema.


Katika mkutano huo Mkazi wa Kijiji hicho Lenisi Jishanga Zengo ameibua changamoto ya uchakavu wa majengo ya Shule ya Msingi Mwalata yaliyojengwa mwaka 1995, yakiwemo madarasa sita na ofisi moja ambayo yanahitaji ukarabati kutokana na uchakavu wake, licha ya changamoto hiyo, shule imeendelea kufanya jitihada kwa kutumia mapato yake ya ndani, ambapo imejenga vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja na sasa imefikia hatua ya kukamilisha boma hivyo ameiomba serikali iwasaidie mapema umaliziaji ili mazingira hayo yawe safi.


Akijibu kero hizo, Mhe. Limbe amesema tayari Wakala wa Usmbazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Kishapu umepitisha bajeti ya Tsh. milioni 50 katika mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kuchimba kisima kirefu na kuweka miundombinu ya kusambaza maji.


"Ndugu zangu Wananchi wa Mwalata nikiri kabisa kuwepo kwa tatizo la ukosekanaji wa maji safi katika eneo letu ila RUWASA bado inasubiria kuletewa fedha hizo na kisha zikifika zitatumika kuanza mradi huo unatarajiwa kujumuisha ufungaji wa umeme wa sola pamoja na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji, hatua itakayosaidia kupunguza adha mnayoipata"Ameongeza Limbe


akijibu swali la Lenisi, Mwenyekiti huyo wa Halmashauri amesema Serikali inaendelea na mpango wa kuboresha miundombinu ya elimu kwa kukamilisha miradi ya zamani na kuanzisha mipya ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.


"Nalipokea hili kisha nitashauriana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Niceforous Mgaya, ili kuangalia uwezekano wa kufanya ukarabati katika shule zenye miundombinu iliyochakaa zaidi, ikiwemo Shule ya Msingi Mwalata kama alivyoaminiwa na Rais wetu nami pia ninaamini utendaji wake suala hilo litakamilika" amesisitiza
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Josephat Limbe akizungumza


Kuhusu changamoto ya umbali wa wanafunzi kwenda sekondari, Limbe amesema Halmashauri kupitia vikao vya Serikali za Vijiji (VDC) vya Mwalata (Ndoleleji) na Masanga (Masanga) imepitisha azimio la kujenga Shule shikizi ya Sekondari katika Kijiji cha Masanga, ndani ya mwaka wa fedha 2026/2027 kwani hatua hiyo inalenga kupunguza umbali wa zaidi ya kilometa 12 ambao baadhi ya wanafunzi wa Mwalata wanalazimika kutembea kwenda Shule ya Sekondari Mangu.


Aidha, kuhusu ujenzi wa Zahanati ya Mwalata ulioanzishwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2015 lakini haujakamilika, Limbe amesema tayari Kijiji kimepokea Sh. milioni tatu kutoka Mfuko wa Jimbo ambazo zimetumika kununua baadhi ya vifaa vya ujenzi.


Ameongeza kuwa alipata nafasi ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI ameahidi kuipatia Halmashauri Sh milioni 60 katika mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kukamilisha zahanati hiyo ili wananchi waweze kupata huduma za afya karibu na makazi yao.


Katika hatua nyingine, Limbe amewashauri wananchi kuwa na moyo wa kujitolea na kushiriki kikamilifu wanapohamasishwa katika uanzishaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akisisitiza kuwa ushirikiano wao ni muhimu katika kuharakisha upatikanaji wa huduma za kijamii.


Pia, amewakumbusha na kuwahimiza wazazi na walezi kuendelea kujitoa kupitia michango ya lishe shuleni ili kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wawapo shuleni, akieleza kuwa lishe bora ni muhimu katika kuboresha afya, mahudhurio na uwezo wa wanafunzi kujifunza.


Akisisitiza dhamira yake ya kuendelea kushughulikia mahitaji ya wananchi wa eneo hilo, Limbe amesema bado anakumbuka ahadi alizozitoa wakati wa kuomba ridhaa ya wananchi na kuwataka kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Wananchi wamepongeza jitihada zinazofanywa na Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji, Niceforus Mgaya, katika kusukuma mbele utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye tija kwa jamii.
Diwani wa Viti Maalumu, Tarafa ya Kishapu, Mhe. Marry Chenge, akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, uliofanyika Kijiji cha Mwalata, Kata ya Ndoleleji, Novemba 3, 2026
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwalata, Daud Yonas, akishiriki mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Josephat Limbe, uliolenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi, Novemba 3, 2026Kaimu Mtendaji wa Kata ya Ndoleleji ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata hiyo, Stanslaus Mussa, akishiriki mkutano wa hadhara wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, uliofanyika katika Kijiji cha Mwalata, Novemba 3, 2026

Mrakibu wa Uhamiaji Cecilia Lucas Matoboki, Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, akitoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya uhamiaji na umuhimu wa kuwa na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Mwalata, Kata ya Ndoleleji, Novemba 3, 2026
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Shija Malisha Ntelezu

Mtendaji wa Kijiji cha Mwalata Halmashauri wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Njile Izengo Kwilasa akifuatilia mkutano huo

Boniphace Saida

Christina Masanja
Peter Kumalija Shija
Gaudencia Jisandu



Lenis Jishanga Izengo

Alex Ntelezu
































































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com