
Shule ya Msingi BECO imefanya vizuri katika Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) mwaka 2026, baada ya wanafunzi wote 42 waliofanya mtihani huo kufaulu kwa kupata Daraja A, sawa na asilimia 100 ya ufaulu.
Kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), shule hiyo yenye namba ya usajili PS1704060 imepata wastani wa alama 275.4762 na kufanikiwa kupata Daraja A (Bora).
Katika matokeo hayo, wavulana 25 na wasichana 17 wote wamepata Daraja A, huku hakuna mwanafunzi aliyepata Daraja B, C, D au E.
Uchambuzi wa matokeo kwa kila somo unaonesha kuwa Hisabati imeongoza kwa wastani wa alama 49.2857 kati ya 50, ikifuatiwa na English Language iliyopata wastani wa alama 48.0000.
Masomo mengine ni Maarifa ya Jamii na Stadi za Kazi (46.4048), Kiswahili (44.3095), Uraia na Maadili (44.1190) pamoja na Sayansi na Teknolojia (43.3571).
Mafanikio hayo yanaonesha matokeo ya juhudi za pamoja katika ufundishaji na ujifunzaji, pamoja na maandalizi ya wanafunzi kuelekea mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.
Uongozi wa BECO Primary School una kila sababu ya kujivunia matokeo hayo, huku mafanikio hayo yakiwa chachu ya kuendelea kuimarisha ubora wa elimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata maarifa na ujuzi unaowawezesha kukabiliana na changamoto za maisha.
Uongozi wa shule unatoa pongezi kwa wanafunzi wote 42, walimu, wazazi na walezi kwa ushirikiano na juhudi zilizochangia kupatikana kwa matokeo hayo.
Hongereni sana BECO Primary School! Wanafunzi 42, wote Daraja A!
TAFUTA HABARI
Social Plugin