Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROF MBARAWA AMPA ONYO MKANDARASI MRADI WA SGR TABORA- ISAKA




Na Sheila Ahmadi, Tabora

Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesemakua Shirika la Reli Tanzania (TRC) linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kiusimamizi na kitaalamu kuhakikisha kipande cha nne cha SGR (Tabora-Isaka),Ujenzi wake unaendelea vizuri.

Waziri Mbarawa ametoa kauli hiyo Oktoba 26 2026 katika eneo la Bukene sehemu mojawapo m ya kipande cha nne cha mradi wa SGR, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi wa SGR kipande cha tatu (Makutopora - Tabora), Tabora- Isaka (kipande cha 4), Isaka- Mwanza (kipande cha 5) na Tabora -Kigoma (kipande cha 6)

Aidha Prof. Mbarawa amempa onyo mkandarasi kampuni ya Yapi Merkezi kwa kushindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati na kuipongeza kampuni saidizi (subcontractor) CCECC, ambayo imetekeleza mradi huo kwa asilimia 5 katika kipindi cha miezi miwili Septemba na Oktoba 2026 sawa na miaka minne iliyotekeleza kampuni ya Yapi Merkezi.

Kutokana na uchelewezashaji uliofanywa na Kampuni ya Yapi Merkezi Prof. Mbarawa, amesema Serikali haitavumilia uzembe wa wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi kwa kasi inayotakiwa, huku akilipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa namna lilivyotumia mkakati mbadala kurejesha kasi ya ujenzi wa reli ya SGR katika kipande cha Tabora–Isaka, chenye urefu wa kilomita 165


Baada ya tathmini kufanyika, Serikali ilibaini kuwa kumwondoa moja kwa moja Mkandarsi huyu kungeweza kuongeza ucheleweshaji na changamoto za kifedha, hivyo akashauriwa kutafuta mkandarasi mdogo mwenye uwezo wa kumsaidia” Alisema Mbarawa.

Profesa Mbarwa, amesema kitendo cha TRC kutia nguvu kiusimamizi na kitaalamu kumesaidia kuongeza nguvu utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha nne ( Tabora–Isaka,) huku kasi ya ujenzi ikiongezeka na kuimarisha matumaini ya kukamilika kwa wakati mwaka mnamo mwaka 2028.

"TRC chini ya Mkurugenzi Mkuu wake, Mhandisi Machibya Shiwa, imefanya kazi kubwa kuweka mazingira wezeshi yaliyomuwezesha mkandarasi kuendelea na utekelezaji wa mradi huo ambao umekuwa ukisuasua na sasa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Watanzania wanashuhudia hali ya mambo katika mradi huo" amesema Prof. Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRC Mhandisi Machibya Shiwa alisema TRC inaendelea kusimamia mradi kwa karibu ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa vifaa muhimu na udhibiti wa matumizi ya fedha ili kuongeza kasi ya utekelezaji.

Kipande cha Tabora–Isaka kina urefu wa kilomita 165 na kina thamani ya dola za Marekani milioni 909.1, ikijumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com