Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AZZA AWAPA MATUMAINI WA WANANCHI WA BUGOGO UJENZI WA BARABARA, AAHIDI UFUATILIAJI ZAIDI



Na Marco Maduhu, Stella Paul, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, amewataka wananchi wa kijiji cha Bugogo Kata ya Mwamala wilayani Shinyanga, wawe na subira juu ya matengenezo ya ujenzi wa barabara ya Bugogo kwenda Usanda, kwamba ameshaongea na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) wilaya ya Shinyanga, na walishafika eneo hilo wakaiona na kuomba wakusanye nguvu sababu eneo hilo kunapaswa kujengwa daraja kubwa na linahitaji fedha nyingi.

TAZAMA VIDEO👇👇


Amebainisha hayo Oktoba 1,2026 wakati akiongea na wananchi wa kijiji hicho, kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitolea majibu.
Azza, amesema wakati anakwenda kwenye kampeni ubovu wa barabara hiyo anaifahamu na kwamba ameshaongeza na watu wa TARURA kwa ajili ya matengenezo na wameshauri wakusanye nguvu ili wajenga daraja kubwa, na hivyo kuwataka wananchi wawe na subira kwasababu hakuna ambaye hatambui umuhimu wa barabara hiyo, bali itatengenezwa.

“Tathmini ya ujenzi wa barabara hiyo ulishafanyika, na nitaendelea kuikumbushia serikali, ili itoe fedha na daraja la Makono liweze kujengwa,” amesema Azza.
Katika hatua nyingine, Mbunge huyo alitoa Sh. 500,000 taslimu kwa ajili ya kununua mashine ya kupiga chapa (photocopy) katika Shule ya Msingi Bugogo, kwa ajili ya kuchapisha mitihani na kuacha kuchangisha wanafunzi fedha za kuchapa karatasi za mitihani.

TAZAMA PICHA👇👇
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bugongo.
Diwani wa Mwamala Hamis Masanja akizungumza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com