Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) KUENDELEA KUJENGA MAKAZI YA GHARAMA NAFUU




Na Sheila Ahmadi, Ruangwa

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuendelea kushirikiana na kampuni mbalimbali pamoja na taasisi za Serikali katika ujenzi wa nyumba na majengo kwa ajili ya wananchi na taasisi nchini.

Hayo yamesemwa na mhandisi Straiton Tibamanya Kutoka kampuni ya Amogtech Mines service baada ya kutembelea banda la (NHC) Ruangwa mkoani Lindi.Bw Straiton alisema kuwa shirika hilo linaendelea kutumia fursa mbalimbali katika kushiriki ujenzi wa nyumba huku likiwa na mpango wa kujenga Ofisi na vituo zaidi katika Maeneo mbalimbali nchini.

lengo la kujenga Miradi hiyo ya nyumba nchini ni kuhakikisha huduma za shirika zinawafikia wananchi wengi zaidi, sambamba na kuweka utaratibu utakaowawezesha wananchi wenye kipato cha chini kupata makazi bora kwa gharama nafuu.

“Shirika hili lipo kwa ajili ya kuwajengea wananchi, hasa wananchi wenye kipato cha chini, nyumba zenye gharama nafuu. Hata kama ni kwa mfumo wa makato, tunataka kuwasaidia kupata makazi ambayo wanaweza kumudu,” amesema Mhandisi Tibamanya"

Aidha shirika linaendelea kujifunza na kuboresha huduma zake ili kukidhi mahitaji ya wananchi, huku likitumia maonyesho mbalimbali, ikiwemo Maonyesho ya Madini, kuwawezesha wananchi kupata taarifa zaidi kuhusu huduma na fursa zinazotolewa.

Vilevile ushiriki katika maonyesho hayo unatoa fursa kwa wananchi na wadau mbalimbali kufahamu huduma zinazotolewa na shirika pamoja na namna wanavyoweza kunufaika na huduma hizo.

Kwa upande wake Mkazi wa Eneo hilo Salha Machel ametoa wito kwa wananchi wengine waendelee kutembelea kwenye banda la Shirika la nyumba ili waweze kupata elimu zinazohusiana na makazi ya wananchi kwani kupitia banda hilo ni huduma mbalimbali zinatolewa bila gharama yeyote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com