Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHAKAMA YAMTIA HATIANI MWENYEKITI WA KITONGOJI MULEBA KWA RUSHWA

 

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mahakama ya Wilaya ya Muleba imemtia hatiani Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busingo ‘B’, kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, Projest Tibishubwamu Frugence, kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Shilingi 22,500 kutoka kwa Said Nasoro Said.

Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU Wilaya ya Muleba, fedha hizo zilitolewa ili kumruhusu Said Nasoro Said kuendelea kufuga mifugo katika Kijiji cha Rwanda, Kata ya Kamachumu.

Katika hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Lilian Mwambeleko (PRM), mahakama imemtoza mshtakiwa faini ya Shilingi 500,000 au kifungo cha miaka mitatu jela, pamoja na kuamuru kurejeshwa kwa Shilingi 22,500 kwa mhanga.

Baada ya kushindwa kulipa faini hiyo, mshtakiwa amepelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu.

Tibishubwamu alishtakiwa kwa kosa la rushwa kinyume na Kifungu cha 15 cha PCCA, Sura ya 329 (R.E. 2023).

 Shauri hilo lenye namba 10966/2026 liliendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Wakili David Mwakyusa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com