Na Mwandishi wetu, Dodoma
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya barabara nchini huku serikali ikiwa imetoa takribani ya Dola Milioni 65 kwa ajili ya kurejesha mawasiliano yaliyoharibika kutokana na mvua za El Nino za mwaka 2023/2024.
Akizungumza na Wanahabari Kwenye Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma mkoani Dodoma Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma Tarura, Catherine Sungura amesema TARURA wanahudumia barabara za wilaya zenye urefu wa Kilomita 144,429 nchi nzima zikiwemo barabara za lami,mawe,changarawe na udongo.
Tunaendelea kujenga Madaraja nchi nzima katika kuhakikisha jamii inapata huduma za maendeleo kupitia barabara hizo hivyo kufikia sasa tunaMadaraja ya Mawe yapatayo 490 .
" Kutokana na mvua Za mwaka 2023/2024 Tarura tulipokea fedha kutoka benki ya dunia takribani ya dola Milioni 65 kwa ajili ya kurejesha mawasiliano ya barabara ambazo ziliathirika na Mvua za Elnino ambapo kwa sasa tumerudisha Mawasiliano ya barabara hizo kwa asilimia 70 katika Vijiji,Wilaya na Mikoa." Amesema Mkuu wa kitengo Sungura"
Aidha, mameneja wa mikoa hususani mkoa wa tabora wilaya ya sikonge na urambo huduma zimerejea kwa wananchi kama kawaida hivyo tarura tunaendelea kuboresha miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa TACTIC katika miji 45 ambapo tunajenga masoko, barabara za lami na Mradi wa DMDp 2 ambao tunajenga takribani kilomita 250 katika wilaya 5 za mkoa wa Dar es Salaam.
Vilevile kwa mkoa wa Dar esalaam tuwatoe hofu Wananchi kuwa wakandarasi wamerejea kukamilisha miundombinu ya barabara hiyo hivyo Mtaa wa majohe kivule kuna kilomita 2 za barabara za zege vilevile kigamboni.
Katika Hatua nyingine tarura tumetoa ajira kwa kikundi cha maafisa usafirishaji (bodaboda) mkoani morogoro wilaya ya ifakara na ambapo wanafanya matengenezo ya kawaida ya miundombinu na hivyo wanaenda kuinuka kiuchumi kupitia miradi wa RISE.
Kwa upande wake afisa utumishi mkuu Speransia Mhapa ameongeza kuwa tarura imefanya mabadiliko mbalimbali kwenye sekta ya miundombinu nchini ambapo tunatambua katika maendeleo hayo watumishi wa umma wamekuwa na mchango mkubwa katika kukamilisha suala hilo la miundombinu.
Nitoe wito Kwa wananchi wote wanaoendelea kutembelea kwenye maadhimisho haya wafike kwenye banda la Tarura kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala wa barabara za mijini na Vijijini (TARURA)

Social Plugin