Na mwandishi wetu, Dodoma
Wizara ya mambo ya ndani Nchini Tanzania kwa mwaka 2026/27, imeliomba Bunge la Tanzania kuidhinisha bajeti ya Jumla ya shilingi trilioni mbili, Bilioni mia nne arobaini na tatu, Milioni mia mbili kumi na tano, laki tisa na ishirini na saba elfu (2,443,215,927,000) kwaajili ya matumizi ya Wizara hiyo.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo, Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Patrobas Katambi, leo Mei 25, 2026, ameliambia Bunge la Tanzania kuwa Wizara yake pia imepanga kukusanya jumla ya shilingi Bilioni mia nne tisini na tisa na milioni tisini (499,090,000,000) kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, akisema Wizara hiyo itaendelea kuimarisha matumizi ya mifumo ya kielektroniki na ununuzi wa vitendea kazi vya kisasa ili kuweza kufikia lengo walilojiwekea.
Kulingana na ufafanuzi wa Waziri Katambi, shilingi trilionj moja, bilioni mia tisa hamsini na tatu, milioni mia tatu sitini na sita, laki nne na themanini na sita elfu (1,953,366,486,000) sawa na asilimia 80 ya bajeti yote ya wizara ni kwaajili ya matumizi ya kawaida.
"Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Moja Themanini na Tatu, Milioni Mia Saba Sitini na Sita, Laki Sita na Arobaini Elfu ni Mishahara na Shilingi Bilioni Mia Saba Sitini na Tisa, Milioni Mia Tano Tisini na Tisa, Laki Nane na Arobaini na Sita Elfu (Shilingi 769,599,846,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo." Amesema Waziri Katambi.
Aidha Shilingi Bilioni mia nne themanini na tisa, Milioni mia nane arobaini na tisa, laki nne na arobaini na moja elfu (489,849,441,000) sawa na asilimia 20 ni kwaajili ya miradi ya maendeleo.
"Kati ya fedha hizo, Shilingi Bilioni Mia Nne Hamsini na Tatu, Milioni Mia Tisa Hamsini na Tano, Laki Nane na Arobaini na Tatu Elfu (Shilingi 453,955,843,000) ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni Thelathini na Tano, Milioni Mia Nane Tisini na Tatu, Laki Tano na Tisini na Nane Elfu (Shilingi 35,893,598,000) ni fedha za nje." Ameongeza kusema Mhe. Katambi.


Social Plugin