Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA MGENI RASMI HAFLA YA KUHITIMISHA MAFUNZO YA MAAFISA NA WAKAGUZI WASAIDIZI 719



Na mwandishi wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe ya Kufunga Mafunzo ya Maafisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Jeshi la Polisi ambayo yamechukua miezi sita ambapo kesho tarehe 28/5/2026 mafunzo hayo yakihitimishwa ambapo wahitimu Mia Saba na Kumi na Tisa wakitarajiwa kuhitimu mafunzo hayo.

Akizungumza baada ya kutembelea na kukagua maandalizi ya shughuli hiyo na maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi, jijini Dar es Salaam ambapo mafunzo hayo yamefanyika, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema ni maboresho makubwa yamefanywa katika Jeshi la Polisi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt.Samia Suluhu akigusia na maeneo mengine yaliyofanyiwa maboresho makubwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com