
Wananchi wa Old Shinyanga wameendelea kusisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu kama msingi mkuu wa maendeleo endelevu katika eneo lao.
Juma Maige mkazi wa eneo hilo amesema kuwa bila hali ya amani, jitihada zote za kiuchumi na kijamii haziwezi kuzaa matunda yaliyokusudiwa,na kuwaomba wananchi kuendelea kuliombea taifa ili nchi iendelee kuwa na utulivu.
Amesema vurugu hazina tija na kila kitu husimama na katika kipindi ambacho kina utulivu shughuli za biashara zinakwenda kwa kasi, huku wawekezaji wadogo na wa kati wakipata fursa ya kuanzisha miradi mbalimbali.
Amesema kuwa hali hiyo imechangia kupunguza umaskini na kuongeza kipato cha familia nyingi katika eneo hilo,imewezesha watoto wao kuhudhuria shule bila hofu, jambo lililosaidia kuinua kiwango cha elimu katika jamii.
Ametoa wito kwa Jamii hasa kupitia kundi la vijana ambao wengi wanakabiliwa na mambo mengi,amewasisitiza umuhimu wa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kulinda usalama wa maeneo yao.
Amesema ushirikiano huo ni silaha muhimu katika kuzuia vitendo vya uhalifu vinavyoweza kuvuruga amani iliyopo.
Amebainisha kuwa utulivu si chaguo bali ni hitaji la msingi kwa maendeleo yao, huku akiahidi kuwa balozi kwa vijana wengine kuilinda amani na kuendelea kulinda hali hiyo kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Social Plugin