Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMANI NI SILAHA YA KUTIMIZA NDOTO NA MAONO YETU- MSIGWA



Na mwandishi wetu, Dodoma

Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amesisitiza umuhimu wa kila Mtanzania kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kulinda na kudumisha amani na mshikamano uliopo nchini kama msingi muhimu unaoweza kumsaidia kila Mmoja kuweza kutimiza ndoto na maono waliyo nayo kwa maendeleo na ustawi wa mtu mmoja mmoja, familia na Taifa kwa ujumla.

Msigwa ameyasema hayo wakati akizungumza ma Chombo kimoja cha habari Mjini Dodoma leo Jumamosi Aprili 10, 2026, akisisitiza kuwa hata matarajio, matamanio na mipango iliyo kwenye Dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 hayawezi kufikiwa bila ya amani, utulivu na mshikamano wa jamii utakaowezesha sekta binafsi na kila Mtanzania kujielekeza katika kuendeleza shughuli za kiuchumi na Kijamii.

"Hatuwezi kufanya kazi kama nchi haina utulivu, niwaombe Watanzania tulinde amani, utulivu na mshikamano wetu kwa gharama yoyote kwani ndoto hizi kubwa za kufikia matarajio na matamanio yetu zitatimia ikiwa tuna amani, utulivu na mshikamano." Amesema Msigwa.

Msemaji huyo wa serikali amesisitiza kuwa Dira 2050 katika kutimiza lengo la kuwa na uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja unategemea sekta binafsi kwa takribani asilimia 70 na sekta ya Umma kwa asilimia 30 pekee, hivyo badala ya kupoteza muda kubishana na kushughulika na mambo ya maana, Msigwa ameomba kila Mtanzania kujielekeza katika uzalishaji mali na kutumia fursa za kiuchumi zilizopo nchini zikivutia zaidi kutokana na amani na utulivu uliopo nchini Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com